NMB mna shida gani kwenye huduma zenu kupitia mawakala?

Champion tz

Member
Joined
Aug 31, 2018
Posts
11
Reaction score
7
NMB huduma za kibenki kupitia kwa mawakala imekuwa ni changamoto.

Unaweza kwenda kwa mawakala hata 5 mfululizo, kila mtu atakuambia mara huduma hamna, mashine hamna etc.
Sijui shida ipo kwa nani.

Yaani kama una shida ya haraka na hela yako lazima ukione cha moto, ukiachilia mbali ATM zenyewe zilivyo chache.

Mnajibrand sana huduma zenu lakini huko kwenye uhalisia ni madudu.
 
Kamisheni inaonekana ndogo. Hiyo changamoto IPO Ina miez kadhaa sasa
 
Kumbe hii shida ipo sehemu nyingi...jana nilikuwa natuma kahela ka mwenye nyumba basi nilizunguka mpaka nikachoka

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
kwamba kwa wakala Mashine hamna?[emoji848]
 
Nimefanya hii kazi ya uwakala kwa muda fulani mfupi. Mchawi ni network tu kwenye vile vipos. Inakera sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…