NMB na CRDB wamejaa Uswahili kwenye huduma zao

NMB na CRDB wamejaa Uswahili kwenye huduma zao

Notorious thug

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2021
Posts
2,817
Reaction score
10,667
Kuna habari nyingi za wateja kuibiwa fedha zao, kadi kumezwa ovyo, mashine kutokutoa risiti, makato makubwa na yasiyoeleweka, huduma mbovu na mambo mengi ya kihuni na ubaya hawajirekebishi bora wateja wahamie EXIM, STANBIC & KCBL
 
Eee Uswahili tena...

Sie Wa Manerumango sijui tulikosa nini?

Wapi kuna Uarabu twende huko?
 
Kila kitu cha mtanzania huwa ni Hovyo hovyo tu,

Hakuna Huduma yeyote inayo tolewa na mtanzania ikakosa dosari.

Ndio maana wawekezaji kama mkurugenzi wa NALA Benjamin Fernandez Ali amua kuweka makao makuu ya kampuni yake Nairobi Kenya.

Sio huku bongo kwa mazwazwa wasio jitambua.
 
Ukaona uje ujjitangaze tukafungue bank acc kwenye hizo orodha za hizo bank [emoji23][emoji23]
 
Kuna siku nilienda kutoa pesa ATM, Mashine ikawa inahesabu, Kadi ikatoka, risiti ikatoka pesa imetolewa, msg kwenye simu inakuja umefanya muamala, halafu Pesa haitokii...

Ilikua mtiti pale, nilizuia Mtu kugusa ile ATM, kuingia ndani naogopa, unaweza upishane nayo unatoka watu wamepita nayo, Nikamuita Mlinzi nikamwambi Aisee asikanyage mtu hapa...

Nikaingia ndani, Mhudumu akaniambia usijali pesa haiwezi tokaa, Nikamwambia Sawa ila ile ATM hakanyagi mtu pale..
Akatabasamu nikatoka nje kuimarisha ulinzi, hakusogea mtu pale mpk walivyokamilisha mambo yao..
 
NMB nimeonba debt clearance tangu Mwaka Jana mpaka leo wananizungusha tu
 
Hizo benki zinatengeneza faida kubwa,ukiwashauri waondoe "processing fee"kwenye mikopo yao wabakie na interest wanazozilamba wamekaza fuvu.
Nimewakimbia.
 
Kuna siku nilienda kutoa pesa ATM, Mashine ikawa inahesabu, Kadi ikatoka, risiti ikatoka pesa imetolewa, msg kwenye simu inakuja umefanya muamala, halafu Pesa haitokii...

Ilikua mtiti pale, nilizuia Mtu kugusa ile ATM, kuingia ndani naogopa, unaweza upishane nayo unatoka watu wamepita nayo, Nikamuita Mlinzi nikamwambi Aisee asikanyage mtu hapa...

Nikaingia ndani, Mhudumu akaniambia usijali pesa haiwezi tokaa, Nikamwambia Sawa ila ile ATM hakanyagi mtu pale..
Akatabasamu nikatoka nje kuimarisha ulinzi, hakusogea mtu pale mpk walivyokamilisha mambo yao..
Hiyo ishawahi nikuta halafu zamani sana, kuna mtu alikua hajui kutumia ATM basi kapata sms kwenye simu yake kurudi nikamwambia pesa haikutoka acha mwanangu huo mtiti, tulipambana mpk tukapata namba ya zone meneja ndo akasema baaada ya siku 3 zitarudishwa ila acha tangu siku hiyo ile ATM siendi kutoa hata hela zangu.
 
Kuna habari nyingi za wateja kuibiwa fedha zao, kadi kumezwa ovyo, mashine kutokutoa risiti, makato makubwa na yasiyoeleweka, huduma mbovu na mambo mengi ya kihuni na ubaya hawajirekebishi bora wateja wahamie EXIM, STANBIC & KCBL
CRDB nilishawahama huduma zao ni mbovu,wana majibu ya ajabu,makato yasiyoeleweka,kusikia mteja kaibiwa hela Crdb ni kitu cha kawaida
 
Back
Top Bottom