NMB Sandbox API

NMB Sandbox API

Rabonn

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2018
Posts
5,789
Reaction score
11,106
Wakuu (wahusika) habari ya jioni.

Samahani kwa usumbufu, lakini nimekua nikiifuatilia sana hii kitu NMB SANDBOX API huduma ya NMB Bank kwa ajili ya staturps/computer developers ambapo wanaweza kuitumia kwenye mifumo yao wanayoi develop ku-utilize NMB financial services.

Kwakweli imekua ikinichanganya sana na ninatamani kuielewa. Nilikata tamaa mpaka leo wadau wa nmb walipo nicheck kwa email mmoja wapo anaitwa Paul Shilla. Then I nikakumbuka kuja atleast kuomba msaada hapa jukwaani kwa wadau wenye uelewa na hii kitu ili wanisaidie kuielewa maana nina uhitaji wa ku-intergrate kwenye shughuli zangu.

Hawa jamaa wa NMB hawajibU e-mail za kuomba assistance za namna hii that is why nimekumbuka kuja hapa jukwaani maana najua wapo wajuvi wa hiz kitu.

I believe ni kitu flan kidogo sanaa I think am messing up but nimekwama kwa muda mrefu sana hapo after trying and trying and trying.

Nikwamueni wakuu.

Ahsanten sana
 
Hii thread yako ungeweka jukwaa la tech nadhani kule utapata Msaada Kwa haraka.
 
Mkuu ku-intergrate nmb kuna changamoto kidogo maana kuna process na inahiji uwe official kwenye operation zako na security ya mfumo wako uwe verified
 
Wakuu (wahusika) habari ya jioni.

Samahani kwa usumbufu, lakini nimekua nikiifuatilia sana hii kitu NMB SANDBOX API huduma ya NMB Bank kwa ajili ya staturps/computer developers ambapo wanaweza kuitumia kwenye mifumo yao wanayoi develop ku-utilize NMB financial services.

Kwakweli imekua ikinichanganya sana na ninatamani kuielewa. Nilikata tamaa mpaka leo wadau wa nmb walipo nicheck kwa email mmoja wapo anaitwa Paul Shilla. Then I nikakumbuka kuja atleast kuomba msaada hapa jukwaani kwa wadau wenye uelewa na hii kitu ili wanisaidie kuielewa maana nina uhitaji wa ku-intergrate kwenye shughuli zangu.

Hawa jamaa wa NMB hawajibU e-mail za kuomba assistance za namna hii that is why nimekumbuka kuja hapa jukwaani maana najua wapo wajuvi wa hiz kitu.

I believe ni kitu flan kidogo sanaa I think am messing up but nimekwama kwa muda mrefu sana hapo after trying and trying and trying.

Nikwamueni wakuu.

Ahsanten sana
Mimi ni mdau ambaye natumia NMB Sandbox na nimeona nishiriki kwenye hii thread kushare na wewe kwa undani taarifa zaidi kuhusu huu mfumo.

Naomba kwa kuanza nitoe ufafanuzi jinsi mfumo unavyofanya kazi na kisha tuangalie wewe binafsi unakwama wapi na ikiwezekana nikusaidie

Kwa nilivyoelewa kuhusu huu mfumo wa NMB Sandbox ni mfumo ambao umewekwa kwa malengo yafuatayo.

Kuwezesha “developers” wanaotengeneza mifumo, kufanya majaribio ya mifumo yao (Hii ndio hiyo sandbox) - NMB Bank API SandboxHome

Ukimaliza majaribio ya mfumo wako na kujiridhisha kuwa unafanya kazi, NMB wanaweza kufanya kazi (Partnership) lakini hili ni lazima lipitie utaratibu wao wa kawaida wa kibiashara na NMB na haimaanishi kuwa kama wewe umefanikiwa kutest basi moja kwa moja utafanya kazi na NMB.

Tukianza na lengo la kwanza kwenye hiyo sandbox hapo juu ni sehemu ya kujaribu tu mfumo wako, data na APIs zote zilizo hapo zina dummy data (Nadhani tunaelewana hapa maana nimeona una degree nne za IT).

Mfumo wao walivyouweka umefuata kitu kinaitwa Open banking Standard (Home - Open Banking) Kwanini? Kwasababu kupitia hizi standard vitu vingi sana vimeshafanyika kwenye upande wa API design na Specifications ya hizo API, hivyo haina haja ya kuifanya hii kazi upya.

Standards hizi zinafocus sana kwenye “openness ya customer data” ambayo ndio future ya bank APIs.

Kwenye sandbox ndo sehemu ya kuanzia na hasa hasa unaanzia kwenye hii link API Explorer – Hapa utapata maelezo kuhusu yafuatayo:

API design iliyo na namna ya kuintagreate,

  • Post request, sample successfully request and responses zikoje lakini pia
  • kuna test accounts ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya tests.
  • Hiyo link hapo juu ni ya muhimu kuliko kitu chochote. Chukua muda wako isome ielewe.

Baada ya test zako zote kukamilika kuna stage ya pili ambayo inaitwa Pre-production environment. Hii ni kama sandbox lakini tofauti yake na Sandbox hii haipo public kwa maana ya kwenye internet.

Access ya hii “second environment” ni lazima wakupe private URL yao ambayo wata-“authenticate request” zako kupitia mTLS. Sasa ili upate hii access ni lazima uwe umetest kwenye sandbox na kuwaonyesha jinsi ambavyo mfumo wako unafanya kazi. Hapa kuna utaratibu wa makubaliano ya biashara na yakikamilika ndo wanakupa access ya kwenda kufanya test pre-production.

Baada ya Pre-production test kukamilika ndo utaweza Kwenda production ambako huko ni live environment.

Mambo ya muhimu

  • Kama umekwama kwenye sandbox kuna support channel ambayo ipo kwenye tovuti yao ya sandbox - Open Bank Project
  • Tengeneza account hapo na uliza maswali maana ni chat forum, wakati mwingine kwenye email majibu yanaweza kuchelewa
  • Ili test zifanyike itabidi uombe permission kadhaa za kufanya hizo requests – zinaitwa “entitlements” ambazo zote unaomba kwenye account page yako ya sandbox.
  • Naomba nisisitize tena, hii link ndo msahafu wa kuanzia - API Explorer
  • Kama iliyo mifumo mingine mingi, mfumo wao haupo perfect, inawezekana kuna design assumptions walizifanya ndani ambazo kwa namna moja au nyingine hazikidhi namna ambavyo application yako iko designed au unataka ifanye kazi. Kwenye hili mnaweza kushauriana nao ili kuweka mambo sawa.
Natumai maelezo haya ya kina yatakupa muongozo mzuri.
 
Back
Top Bottom