Nmb yapata ceo mpya

Nmb yapata ceo mpya

huyu CEO anayeondoka hajafanya vizuri kabisa. NMB inajulikana kama "the sleeping giant". Ni aibu hii benki. Ina bahati sana kwa kuwa ni kubwa by default. Mishahara ya wafanyakazi wa serikali inapitia pale. kama ingekuwa wafanyakazi wa serikali wanauhuru wa kuchagua benki wanaoitaka basi ingekuwa shughuli.

hii benki inamiliki sehemu nyingi tokea zamani lakini bado inashindwa na crdb bank ambayo inapanga sehemu kibao. wao town centre dsm wana branch 2, wakati wenzao wana 5

halafu uongozi wao wote umejaa wageni kasoro CFo waziri
nadhani unaongea tu bila kufuatilia kiundani, huwezi kulinganisha NMB na CRDB kwani hata kwa idadi ya matawi NMB imeizidi CRDB sana ndio maana NMB inashinda tender ya kuhudumia watumishi wa serikali kwa kuwa ina mtandao mkubwa sana na pia ndio bank inayoongoza kwa kuwa na capital kubwa nchini, umiliki wa majengo ni asset kubwa sana kwa NMB na ndio inayoifanya iwe strong financially. NMb ina matawi sehemu zote muhimu mjini na wala haibagui maeneo kama baadhi ya benki na ndio siri kubwa ya kushinda tender za serikali.

Ukiongelea city centre NMB wana tawi kubwa tu pale NMB House na pia kuna branch ya kubwa sana ya Bank House na pia kuna matawi kama Morogoro Road, Kariakoo, Muhimbili, Ilala, Magomeni, Ubungo, Mlimani City, Mwenge, UDSM, Temeke, Mbagala, Masaki, Mikocheni to metnion the few

Hii benki ni kubwa na ndio inayoongoza kwa nchi yetu mie si mteja wa hii benki ila nadhani ndio benki iliyofanikiwa baada ya kubinafsishwa kuliko benki zote. Benki kama CRDB inajitangaza sana na ni kubwa na ni mfano kwa kuwa inaongozwa na wazalendo lakini uwezi fananisha na NMB hata kidogo
 
Ni aibu hii benki. Ina bahati sana kwa kuwa ni kubwa by default. Mishahara ya wafanyakazi wa serikali inapitia pale. kama ingekuwa wafanyakazi wa serikali wanauhuru wa kuchagua benki wanaoitaka basi ingekuwa shughuli


kwa mfano tenda ya kupitisha mishahara ya JESHI TPDF, CRDB na NMB waligombania hiyo tenda , na NMB wakashinda kwa kuhaidi kufunga ATM , Katika kambi zote za Jeshi DAR, na baadhi ya Mikoa, na wanajeshi kuhaidiwa kupewa mikopo mikubwa ya wafanyakazi, kuringanisha na wafanyakazi wengine
 
Tunamtakia heri na mafanikio ceo mpya wa nmb.taasisi za bank za afrika zinachangamoto mbalimbali, hasa uhaba wa rasili mali mitaji na uwekezaji mdogo wa mitaji hasa katika viwanda na kilimo. Pamoja na faida ipatayo nmb, mishahara ya watumishi,hupitia tu benki na wenye yao huichukua kwenda kutumia.
 
NMB yapata Mkurugenzi mpya Send to a friend Wednesday, 12 January 2011 20:14


wiessingnmb.jpg
Mark Wiessing

Furaha Maugo
BODI ya wakurugenzi ya Benki ya Makabwela (NMB), imemteua Mark Wiessing kushika wadhifa wa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki hiyo.

Wiessing ameshika nafasi hiyo kutoka kwa Ben Christiaanse ambaye amememaliza muda wake wa miaka minne.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Bodi ya NMB Misheck Ngatunga, alisema Wiessing ni mchapakazi na ana uzoefu.

“Anakuja na uzoefu mkubwa wa masuala ya kibenki, uzoefu alioupata sehemu kubwa ya Afrika na sehemu nyingine duniani hasa katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na ongezeko kubwa la ushindani katika soko,” alisema Ngatunga.

Wiessing(52)kabla ya kushika wadhifa huo amewahi kuwa mkurugenzi mtendaji wa Benki Taifa ya Biashara Zambia(ZANACO),Standard Charted nchini Afrika Kusini, amewahi pia kuwa ,Mkurugenzi wa Kanda ya nchi za Afrika Magharibi katika shughuli za kibenki.
Amewahi kuwa Mratibu wa City Bank nchini Ivory Coast, amefanyakazi nchi za Ulaya Mashariki,Kusini Mashariki mwa Asia na kampuni ya IGP.
Ana Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara aliyopata chuo kikuu cha USA.
Benki ya NMB ilianzishwa mwaka 1997 lakini mwaka 2005 ilibinafsishwa baada ya serikali kuuza asilimia 49 ya hisa zake kwa Rabobank.
Mwaka 2008 serikali ilipunguza tena hisa zake hadi kufikia asilimia 30, kwa kuuza hisa za asilimia 16 kwa wananchi na asilimia 5 kwa wafanyakazi wake, ambapo mwaka huohuo iliorodheswa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
 
Sawa kabisa, kazi kubwa ya CEO is to make sure investers interest are safeguarded. Hawalaziki kumtoa sehemu yoyote!
 
Back
Top Bottom