Nmeibiwa simu, kesi iko mahakamani. Maswali gani ya kumuuliza mtuhumiwa?

Nmeibiwa simu, kesi iko mahakamani. Maswali gani ya kumuuliza mtuhumiwa?

Hakikisha kwanza una risiti halali ya hiyo simu yako, na namba ilisajiriwa Kwa jina lako.

Kisha pika mashaidi Hata watatu wanaweza kuishawishi mahakama.

Pia andaa pesa mkono mtupu haulambwi.
 
Hapo simu umeibiwa, usumbufu utaupata na fidia utalipa unless huyo unayempandisha kizimbani hajielewi.!!
Sio kila kesi mtu anayoshindwa anamlipa fidia.

Unless mshtakiwa athibitishe kwamba palikuwa na malice prosecution. Na kuthibitisha malice prosecution lazima ku establish some important ingredients of malice.
 
Wakuu mimi kuna mtu aliniibia simu yangu usiku wa saa tisa nilimuona dirishani(kuna taa imefifia mwanga lakini unaweza kumuona mtu na mlangoni(pale mlangoni kuna ka duara hivi kwahiyo kabla ya kufungua mlango nilimuona na penyewe kuna taa ambayo inamulika vizuri) sasa zikapita siku nikawa namuona sehemu. Ikabidi niende kumshtaki.

Wakauliza anapokaa anasema mtaa ule ule ninaokaa mimi, ila kijana akakataa kata kata kwamba siyo yeye, wakati yeye ndiye niliyemuona ila anabisha. Basi wakasema kesi ipelekwe mahakama. Ndiyo tunasubiria week ijayo.

Vipi ni maswali gani ya kumuuliza mtuhumiwa?
Hiyo simu ina thamani gani mpaka uende mahakamani? Una ushahidi gani zaidi ya "nilimuona"?
 
N
Hii kesi unashindwa, hata kama ukimkuta na simu bado unashindwa

Haswa kwenye swala la utambuzi, unapaswa uishawishi mahakama beyond reasonable doubt kuwa ni yeye na sii mwingine, kwanza unapaswa uieleze mahakama ni kwann ulikua macho saa tisa usiku na ikawaje ukawa unaangalia hayo maeneo ambayo mwizi angeweza kufanya jambo, na je alipoiba uliona au haukuona?

Reaction yako ilikuwa nn baada ya ulichokiona? Usiwaze sana kitu cha kumuuliza, waza sana ni kwa namna gani unaweza kujenga hoja ikaeleleweka kwanza.
Nilikuwa nmelala. Baadae nikawa kama nmeshikwa na kitu mguuni, kushtuka kuangalia dirishani, dirisha liko wazi,simu ilikuwa upande wa miguuni wa kitandani karibu na dirisha. Kwahiyo ile nashtuka moja kwa moja naangalia dirisha liko wazi simu haipo. Nikasimama kitandani ndipo nikamuona mwizi, nikaanza kushtuka simu yangu, simu yangu, aliponiona akajibanza kwenye ukuta, nikawa namwambia kaka naomba simu yangu, akasema leta hela laki na hamsini nikamzungusha hapo wee baadae nikamwambia sawa nakupa. Nmetoka nje( getini mlangoni katikati kuna mduara mkubwa nikachungulia kabla ya kufungua geti, nikamuona na yeye kama alikuwa anataka kufungua geti) basi aliponiona tena akaondoka kuelekea gizani, nikafungua mlango yeye tayari yuko gizani huko. Hivyo ndivyo nilivomuona. Na pale getini kuna taa kubwa kabisa inamulika geti.
 
Ushahidi wa kumuona yeye kama yeye. Ujue mwanzoni niliamuaga kupotezea ila nikawa namuona yaani roho inananiuma, nikaenda kuwaambia police wakaja kumkamata.
Hiyo simu ina thamani gani mpaka uende mahakamani? Una ushahidi gani zaidi ya "nilimuona"?
 
Hapo kwenye utambuzi ndio shida sidhani kama una IMEI NO AU SERIES NO...Kwenye Risiti yako ya Simu.....!! Hapo ndio ugumu ulipooo
 
Baadae hiyo hela aliyokuwa anaitaka sikumpa. Akatokomea gizani. Ndiyo nikarudi ndani ikabidi niite watu, nikachukua simu zao kujaribu kuipigia simu yangu akapokea huyo kaka namwambia naomba simu yangu anasema “naomba uchi”. Baadae tukawa tunapiga simu haipatikani. Ndiyo asubuhi nikaenda kurenew line
 
Sio kila kesi mtu anayoshindwa anamlipa fidia.

Unless mshtakiwa athibitishe kwamba palikuwa na malice prosecution. Na kuthibitisha malice prosecution lazima ku establish some important ingredients of malice.
Malice presecution ni nini mkuu?
 
Ushahidi wa kumuona yeye kama yeye. Ujue mwanzoni niliamuaga kupotezea ila nikawa namuona yaani roho inananiuma, nikaenda kuwaambia police wakaja kumkamata.
Ushahidi wa kumuona tu, tena wewe peke yako hautoshi. Swali jingine, umepeleka kesi ya madai au ulienda polisi wakamshtaki kwa kesi ya jinai?
 
Ushahidi wa kumuona tu, tena wewe peke yako hautoshi. Swali jingine, umepeleka kesi ya madai au ulienda polisi wakamshtaki kwa kesi ya jinai?
Me nilimpeleka police, kesho yake wakasema kesi inaenda mahakamani. Sasa sikujua ni ya madai au ya nini
 
Ongea vizuri na polisi - wampe kile kipigo chao - yeye mwenyewe mwizi ataonyesha alipoiweka hiyo simu, na ataileta mahakamani. Hapo utashinda kesi ki-rahisi kabisa. Mwizi huwa hakubali ki-ulainilaini - hata ukimkamata laivu..
 
Hiyo simu ina thamani gani mpaka uende mahakamani? Una ushahidi gani zaidi ya "nilimuona"?
Ongea vizuri na polisi - wampe kile kipigo chao - yeye mwenyewe mwizi ataonyesha alipoiweka hiyo simu, na ataileta mahakamani. Hapo utashinda kesi ki-rahisi kabisa. Mwizi huwa hakubali ki-ulainilaini - hata ukimkamata laivu..
Ongea vizuri na polisi - wampe kile kipigo chao - yeye mwenyewe mwizi ataonyesha alipoiweka hiyo simu, na ataileta mahakamani. Hapo utashinda kesi ki-rahisi kabisa. Mwizi huwa hakubali ki-ulainilaini - hata ukimkamata laivu..
Huyu kaka ndiye aliyeichukua simu. Mimi siyo mjinga nimsingizie jamani. Siku yenyewe nilimwambia kaka me sitaki chochote zaidi ya hiyo simu. Hata kama ameiuza angeniambia tu kamuuzia nani me nitajua nitafanya nini. Lakini alikataa jamani kwamba hajachukua aisee
 
Huyu kaka ndiye aliyeichukua simu. Mimi siyo mjinga nimsingizie jamani. Siku yenyewe nilimwambia kaka me sitaki chochote zaidi ya hiyo simu. Hata kama ameiuza angeniambia tu kamuuia nani me nitajua nitafanya nini. Lakini alikataa jamani kwamba hajachukua aisee
Kazi ndogo sana hiyo kwa wapelelezi wa polisi...toa tu ushirikiano kwao..
 
Sikumona gizani jamani. Nilimuona kwenye mwanga, tena mara mbili. Labda nilikosea kumpeleka police. Lakini YEYE NDIYE KACHUKUA SIMU YANGU.. hataki kukubali, sema sina ushahdi wa kutosha kwamba nilimkamata nayo au vipi. Lakini nilimuona. Yeye ndiye ameichukua. Anajifanya kukataa tu
 
Kama haiwezekani niambieni nifanyaje tu ili kesi iishe maana mwisho wa siku naona kama sitoipata. Na sikutegemea kwenda mahakamani. Wenyewe askari ndiyo waliipeleka.
 
Back
Top Bottom