Kwa budget ya 6.5M hadi 7M kupata izo gari inawezekana. Ila zitakua katika hali ya kawaida (zimetumika kwa zaidi ya miaka 2 hapa Tanzania).
Ila sikushauri hiyo Mark II Grande kwakua itakusumbua katika Mafuta kama kipato chako ni cha kawaida. Ila kama haitakua issue ichukue ni nzuri.
Tenga muda (mwezi au week 3) fanya research utapata. Usiende showroom hutapata kwa hiyo bei wala usiuziwe na madalali wanaongeza cha juu sana.
Sehemu za kutembelea: jamiiforums jukwaa la matangazo na biashara, kupatana (siwaamini wengi wauzaji madalali), facebook groups (hapa ndio yapo mengi na active sana na wauzaji ni madalali na owners).
Ila uwe mvumilivu kutembea kwenda kukagua gari ukiwa na fundi au mtu mwenye ujuzi wa magari, mnaejuana sana na unamuamini. Mafundi wengine iwa wanakonyezwa na muuzaji palepale hafu anakuambia gari zuri nunua yeye baadae anapewa cha juu wewe linakufia unadhani ni bahati mbaya kumbe gari ilikua kimeo.
Angalia other options:
vitz new model
IST
Raum
Ila kama hela ya mafuta ni ya mshahara wa kawaida, angalia sana ishu ya engine size.