Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
- Thread starter
- #81
There u go... Choice is all what matters.. Then tusijione bora kwakuwa labda tunaishi mahala fulani...
Ngabu hakuna asiyejua unavyopenda kuwabeza wala vumbi humu. Na hicho ndicho kimejenga tabaka humu la wala vumbi na wabeba box.. Ile mara unatuwekea neighborhood, mara sijui unakula nini wengi wanaona kama unarusha madongo flani kwa watu..
Duh...aisee.
Sasa basi ngoja nikueleze kitu maana nadhani umeyakutia humu haya mambo ya wala vumbi vs wabeba maboksi.
Kwanza nianze kwa kusema hivi, wewe unaona ya upande mmoja tu. Kejeli dhidi ya wala vumbi.
Lakini kejeli dhidi ya hao wanaoitwa wabeba maboksi huzioni. Sana sana nadhani huwa unazifurahia. Tena wenyewe mkiziona sehemu huwa mnaitana kabisa. Ikitokea mmoja wenu kaziona sehemu na asiwaite wenzie, hampendezwi.
Nirudi kwenye hilo unaloliita tabaka la wala vumbi na wabeba maboksi. Iko hivi, kuna wakati fulani, kitambo kidogo, kejeli dhidi ya Watanzania waishio ughaibuni zilizidi.
Wanaughaibuni wote wakawa wanaitwa wabeba maboksi. Wakawa wanapondwa humu jamvini. Sasa wengine tukaona isiwe tabu. Kwani kubeba boksi kuna ubaya gani? Kama siji kwa mamako kuomba hela ya chumvi, mimi nikibeba boksi au nikitawadha wazee, wewe shida yako nini hasa hadi uanze kunibeza mimi?
Ndipo watu tulipoanza kulikumbatia hilo jina la wabeba maboksi hadi likabeba maana tofauti na ya mwanzo - ya watu waliokuwa wanafanya hizo kazi kwenye maghala [warehouses] huko. Jina likabeba maana ya watu waishio ughaibuni bila kujali wanafanya shughuli zipi.
Baadhi yetu sasa ndo tukaja na jina la Watanzania waishio Tanzania wawapondao ndugu na jamaa zao walioenda kujitafutia maisha nchi za nje.
Sasa sijui wewe unaona ni poa tu kwa Watanzania waliopo Tanzania kuwaponda Watanzania wenzao walioko nchi za nje. Kama unaona hilo ni sawa, basi sawa. Lakini linakuonyesha jinsi ulivyo kama mtu.
Kwa hiyo sasa ndo watu tukaja na hilo jina la wala vumbi. Kwamba, wewe ukiwa Tanzania halafu ukaanza kukebehi na kukejeli Watanzania wenzako walioko ughaibuni na kuwaita hawana lolote ni wabeba maboksi tu, basi na sisi tutakukejeli kwa kukuita wewe ni mla vumbi uliyepigika na maisha na unajipa faraja katika kuponda wenzio.
Hapo ikawa ngoma droo. Ndipo hayo majina yaliposhika kasi humu na kwenye ile blogu ya Michuzi.
Sasa nije kwangu mimi binafsi. Hayo majina kwangu yamekuwa ni ya kimatani zaidi. Mtu akiniita mbeba maboksi wala sitokwi povu tena. Kwanza napenda kuitwa mbeba maboksi...na ukiliongezea darizi kwa kuniita Rais wa wabeba maboksi ndo nafurahi zaidi.
Hivi hujawahi kujiuliza hata kwa nini najiita rais wa wabeba maboksi? Ingia kwenye profile yangu uone. I take pride in it.
Kwa hiyo mimi binafsi nikikuita wewe mla vumbi, sikuiti hivyo kwa kukudharau wala kukukebehi. Nakuita hivyo kimatani tu.
Tatizo naloliona kwako na kwa wengine labda ni la tone. Wakati mwingine kuijua tone ya mtu kupitia maandishi ni vigumu. Laiti kwa mfano ingetokea mimi na wewe tutakutana sehemu ana kwa ana, kwako ningejitambulisha kama rais wa wabeba maboksi. Ni utani tu. Si zaidi, si pungufu ya hapo.
Mimi nimezaliwa Tanzania. Nimekulia Tanzania. Nimesomea Tanzania. Mama yangu naye vivyo hivyo. Marehemu baba yangu naye alizaliwa Tanzania, kafia Tanzania, na kazikwa Tanzania.
Hivi kwa akili yako kabisa unadhani mimi naweza kuwadharau wazazi wangu kwa kuwaita wala vumbi? Na hata wao hawawezi kunidharau mimi kwa kuniita mbeba maboksi. Hii ya humu JF siku zote mimi nimekuwa nikiichukulia kama utani tu.
Mimi ni mlipa kodi mzuri kabisa wa Tanzania. Hivi kabisa huu utani wa mimi mbeba maboksi na wewe mla vumbi, wewe na wenzako huwa mnauchukulia serious kivile?
Nyie mnataka muwaite wenzenu wabeba maboksi halafu hamtaki kuitwa wala vumbi? Mkiitwa wala vumbi mnachukia? Mnadhani kweli tunamaanisha? Kaazi kweli kweli.
Mbona mimi nimeukumbatia ubebaji boksi hadi nimekuwa rais wao....au hujawahi kuona nikiitwa rais wa wabeba maboksi humu?
Hayo ya mapicha ya ma neighborhoods na sijui ma nini nini huko ni changamsha baraza tu. Sirushi madongo kwa yeyote yule. Kwanza namjua nani humu hadi nimrushie madongo? Na nitafaidika na nini mwisho wa siku?
So there you have it. Mimi mbeba maboksi, wewe mla vumbi.
It's all in jest. Nothing that serious dude.
Be easy!