No referendum for ZNZ; Yes for Unity Government!

No referendum for ZNZ; Yes for Unity Government!

Dondoo 5 za hoja ya msingi ni -
1. BLW liyaridhie na kuyapa nguvu Maridhiaano.
2. Uanzishwe mfumo serikali ya Umoja wa Kitaifa itayohusisha vyama vya siasa vyenye wajumbe ndani ya BLW.
3. Serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa izingatie uwiano kwa mujibu wa kura za urais.
4. Baraza lifanye marekebisho ya vifungu vya 39, 42 na 62 ili kuweka utaratibu wa serikali ya Umoja wa kitaifa.
5. Baraza liweke utaratibu wa kura za maoni, referendum.
 
Jifunze historia utajua kuwa kabla ya kuwepo Tanganyika kulikuwepo na falme, city-states na tawala mbalimbali.. na Kilimanjaro nusura waombe kuwa taifa huru...kabla ya sehemu nyingine za Tanganyika!!

Does this equates zanzibar with kilimanajro in a current situation and status! NO

Unatakiwa ukajifunze historia ya Tanganyika na Zanzibar..kabla ya kufanya argument zilizopinda...
 
Kimsingi.. BLW halitapitisha serikali ya umoja wa kitaifa bali itaridhia kufanyika kwa kura ya maoni. I got it.
 
Hatima ya yote haya ni JK kuisimamia, kuilinda na kuitetea KATIBA ya JMT.
 
Hoja imeshasomwa, majadiliano yanaanza, wa kwanza kuchangia ni Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar. Mhe. Ameanza kwa kupiga nyundo baadhi ya mapendekezo ya huja husika. Amesema hoja zote anazoziunga mkono ni zile tuu zilizoko kwenye sera ya CCM, hivyo wananchi lazima washirikishwe kwa njia ya kura ya maoni.

.

Sawa nami nakubali kura ya maoni. hiyo kura ya maoni wananchi wanaulizwa nini? Maana watu wameshabikia kura ya maoni bila kusema nini kinachopigiwa kura. Watawauliza wananchi mnataka serikali ya umoja? Ndio au Hapana. That will be ridiculous.

CUF na CCM wote akili zao ni POWER tu ndio maana hawafikirii mbali. Ilipaswa wandike katiba mpya yenye vipengele vya serikali ya umoja wa kitaifa na kisha hiyo katika ndio ikapigiwe kura ya ndio au hapana. Pia ni lazima wapitishe sheria kuhusu kura ya maoni na vipengele gani vya katiba havitabadilishwa bila ya kuwa na kura ya maoni. Vinginevyo wanacheza tu makida
 
Waziri kamaliza kwa kushauri mambo yote yafanyike kabla ya uchaguzi mkuu, hivyo hiyo serikali ya umoja wa kitaifa ije baada ya uchaguzi.

Spika Kificho amempongeza waziri kwa kujibu hoja bila jazba.

Sasa anachangia Waziri Samia Suluhu Hassan, ameanza kwa kumpongeza mtoa hoja, amesema anaiunga mkono kwa sababu hoja ya msingi na baadhi ya mapendekezo yako kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM.
 
Kimsingi.. BLW halitapitisha serikali ya umoja wa kitaifa bali itaridhia kufanyika kwa kura ya maoni. I got it.
swali langu lipo pale pale. kura ya maoni kuhusu nini? Wazanzibari wataulizwa nini ili wachague nini? Kwa mazingira gani ya kikatiba? sielewe kabisa kwa nini maswali haya muhimu hatujiulizi
 
Sasa anachangia Waziri Salma Suluhu Ally, ameanza kwa kumpongeza mtoa hoja, amesema anaiunga mkono kwa sababu hoja ya msingi na baadhi ya mapendekezo yako kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Huu U-CCM na U-CUF hautawafikisha mbali kwenye hili! Maslahi ya Zanzibar na wazanzibari yanapaswa kuwekwa mbele ya maslahi ya vyama.
 
I strongly support having one union government instead of two or three governments for the following reasons:

One government will give people a sense of unity instead of us against them. If all Tanganyikans and Zanzibaris worked together under one government it will really strengthen a sense of unity. If formulated properly all will feel like equals.

One government would be cheaper than any other option. We should concentrate our time and resources for other problems. Even if the initial union agreement had problems this shouldn't have been a problem to last over forty years.

I think the root problem of all union matters is the size and population of both nations. Zanzibaris feel outnumbered and outsized and that is usual a cause of establishing like a defence mechanism. I think most Zanzibaris feel that if everything was done together they would be swallowed by Tanganyikas size. This wouldn't be a problem if we had a strong sence of Utanzania.

My take: I think if there is no solution to union problems then we should all count our losses and see how we would divide all the assets. I don't advocate a break in the union the same way no one advocates for a divorce but I believe it reaches a point where a "breakup" is the only option. Both sides should sit down and give reasonable demands and be ready to compromise. If one or both sides are not ready to do that then hey let's just call it a day and move on.
 
Kimsingi.. BLW halitapitisha serikali ya umoja wa kitaifa bali itaridhia kufanyika kwa kura ya maoni. I got it.

Mzee Mwanakijiji, hata mimi mwanzo nilidhani hivyo kuwa CCM itakataa kuanzishwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, ila mood niliyoiona humu, CCM, CUF lao moja, Baraza litaridhia uanzwishaji wa serikali hii ya umoja wa kitaifa ila litaweka referendum as a precondition.
 
"4. Baraza lifanye marekebisho ya vifungu vya 39, 42 na 62 ili kuweka utaratibu wa serikali ya Umoja wa kitaifa."

Kwa faida a yote hivi vifungu vina semaje haswa? Ili wote tujue ni nini haswa kina taka kufanyiwa marekebisho.
 
tunashukuru kwa msaada wako pasco.. tuhabarishe mkuu.. hebu tuambie hapo nahodha na shamhuna wapo? na wanaonekana wako ktk hali gani? na vp spika haoneshi kuwepo upande wowote?
 
Baada ya michango ya mawaziri hao wawili, sasa ni zamu ya CUF, Mh. Mhuzi, ameanza na kuhimiza umuhimu wa serikali ya umoja wa kitaifa from historical perspective, akatolea mfano chaguzi zote kabla ya uhuru, ASP ilipata kura nyingi, 54% lakini viti vichache, ndio maana wakafanya mapinduzi matukufu. Alimtaja John Okello ambaye alikubali serikali ya umoja wa kitaifa lakini pia akamtaja na Sheikh Thabit Kombo aliyepinga serikali ya mseto, hivyo akatoa angalizo kama wote wanakubali serikali ya umoja wa kitaifa, wananchi wakahamasishwa waikatae, matokeo nyakiwa ni kuikataa, then Zanzibar hapatakalika.

Mhunzi amesema hiyo ya majimbo ni deal, kwenye maeneo ya waarabu, waliweka majimbo mengi, na maeneo ya waswahili na washirazi, majimbo machache, huu ameulezea kuwa ni udhalimu, ameomba usiendelezwe.

Mhunzi amesema Karume anaweza kuanzisha serikali ya mseto kwa kuwateua mawaziri toka CUF, bila kuvunja katiba, hivyo amepinga hoja ya serikali ya mseto kusubiri referendum, ametolea mfano mambo makubwa zaidi yaliyofanyika bila referendum, kwanini hili?.

Alipokuwa akizungumzia hoja ya kumuongeza muda Karume, jazba ilimpanda alipozungumzia kutowasikiliza viongozi wa dini, jamaa machozi yalimtoka!, akasema kama wanaitakia mema Zanzibar, hili hawawezi kushindwa kuliona.

Spika anatoa nafasi moja kwa CUF na moja kwa CCM. Line up ya wachangiaji wa CCM ni mawaziri zaidi.
 
Saa hizi ni saa Saba Kasoro, Sauti ya Adhana inasikika, Baraza limenyamaza kimya kuisubiri ipite, sasa anachangia mchangiaji wa mwisho mchana wa leo. Huyu ni Haji Mtema Haji, Mwakilishi wa Koani, CCM, amesema haungi mkono hoja hii jinsi hivyo jinsi ilivyo.

Amesema wanataka kutambua hayo maridhiano ni nini, hivi nini haswa walichozungumza ni nini haswa ambavyo wanataka BLW liliridhie maridhiano gano hayo ya siri. Baraza liridhie siri za watu moyoni?.

Amemponda Karume na Seif kwa kukaa kuficho, kuibuka bila kusema wamekubaliana nini haswa ambacho kimeletwa barazani kiridhiwe.
 
Kwa mtazamo wangu, na kama wengi walivyobaini, ni kwamba referendum inapendekezwa ili kufanya mambo machache. Nayo ni:

1. Kujua hali ya kisiasa kwa vyama viwili vinavyopingana ZnZ. Na hivyo kuweza kubaini matokeo ya uchaguzi mkuu ujao

2. Kuchelewesha makubaliano ya uundwaji wa serikali ya mseto na wakati huo huo kutoa matumaini yasiyokuwepo kwa CUF na wananchi wa ZnZ.

Nadhani kama nia ya kuunda serikali ya mseto ipo, hakuna haja ya kuchelewesha uundwaji wa serikali hiyo. Kikatiba, CCM hailazimiki kuunda serikali ya mseto. Kwahiyo nia yoyote ya kuunda serikali ya mseto inategemea makubaliano ya pande mbili zinazohusika na wala si maamuzi ya wananchi.
 
Patamu hapa kwa MAKAMU wa RAISI,CCM wanataka wawepo makamu wawili wa RAISI,na CUF wanataka makamu MMOJA tu,CCM wanataka inapotokea RAIS hayupo kwa njia yoyote ile,basi makamu wa PILI wa raisi ndio akaimu kiti,CUF wanataka awepo MAKAMU MMOJA tu(ambao wanategemea wataikamata nafasi hiyo) basi akaimu nafasi hiyo mara moja,mnasemaje hapa,ingawa hesabu ya CCM siielewi kabisa.
 
Haji Mtema anaendelea kutema, amesema serikali ya mseto sio suluhu, mbona Kenya na Zimbabwe hazijasaidia. Amesema siasa za visa, uhasama na chuki, Zanzibar ndio jadi yao. Dawa ameshauri ni kuridi kwenye mfumo wa chama kimoja. Hapa amesema hakuna cha serikali ya kitaifa, tuukatae mfumo wa vyama vingi Unguja vinatuumiza, dawa ni kurudi mfumo wa chama kimoja iundwe serikali ya kitaifa chini ya chama kimoja ndio sahihi kwa Wanzanzibari " mambo haya ni mazito, tuyafanye taratibu, haraka haraka haina baraka, mwenye pupa hadiriki kula tamu".

Anasema hilo wazo la chama kimoja likishindikana, basi wanachi waulizwe, wakikubali, sawa, ila hata hiyo serikali ya umoja yenye vyama vingi, anaona bado itakuwa ni fujo tuu.
 
Back
Top Bottom