Baada ya michango ya mawaziri hao wawili, sasa ni zamu ya CUF, Mh. Mhuzi, ameanza na kuhimiza umuhimu wa serikali ya umoja wa kitaifa from historical perspective, akatolea mfano chaguzi zote kabla ya uhuru, ASP ilipata kura nyingi, 54% lakini viti vichache, ndio maana wakafanya mapinduzi matukufu. Alimtaja John Okello ambaye alikubali serikali ya umoja wa kitaifa lakini pia akamtaja na Sheikh Thabit Kombo aliyepinga serikali ya mseto, hivyo akatoa angalizo kama wote wanakubali serikali ya umoja wa kitaifa, wananchi wakahamasishwa waikatae, matokeo nyakiwa ni kuikataa, then Zanzibar hapatakalika.
Mhunzi amesema hiyo ya majimbo ni deal, kwenye maeneo ya waarabu, waliweka majimbo mengi, na maeneo ya waswahili na washirazi, majimbo machache, huu ameulezea kuwa ni udhalimu, ameomba usiendelezwe.
Mhunzi amesema Karume anaweza kuanzisha serikali ya mseto kwa kuwateua mawaziri toka CUF, bila kuvunja katiba, hivyo amepinga hoja ya serikali ya mseto kusubiri referendum, ametolea mfano mambo makubwa zaidi yaliyofanyika bila referendum, kwanini hili?.
Alipokuwa akizungumzia hoja ya kumuongeza muda Karume, jazba ilimpanda alipozungumzia kutowasikiliza viongozi wa dini, jamaa machozi yalimtoka!, akasema kama wanaitakia mema Zanzibar, hili hawawezi kushindwa kuliona.
Spika anatoa nafasi moja kwa CUF na moja kwa CCM. Line up ya wachangiaji wa CCM ni mawaziri zaidi.