Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Patamu hapa kwa MAKAMU wa RAISI,CCM wanataka wawepo makamu wawili wa RAISI,na CUF wanataka makamu MMOJA tu,CCM wanataka inapotokea RAIS hayupo kwa njia yoyote ile,basi makamu wa PILI wa raisi ndio akaimu kiti,CUF wanataka awepo MAKAMU MMOJA tu(ambao wanategemea wataikamata nafasi hiyo) basi akaimu nafasi hiyo mara moja,mnasemaje hapa,ingawa hesabu ya CCM siielewi kabisa.
Dondoo 5 za hoja ya msingi ni -
1. BLW liyaridhie na kuyapa nguvu Maridhiaano.
2. Uanzishwe mfumo serikali ya Umoja wa Kitaifa itayohusisha vyama vya siasa vyenye wajumbe ndani ya BLW.
3. Serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa izingatie uwiano kwa mujibu wa kura za urais.
4. Baraza lifanye marekebisho ya vifungu vya 39, 42 na 62 ili kuweka utaratibu wa serikali ya Umoja wa kitaifa.
5. Baraza liweke utaratibu wa kura za maoni, referendum.
.asante sana mkuu kwa kutu update,ila ujasema baadhi ya watu kama Shemhuna wakoje?na unaonaje upopo wa kisiasa upoje hapo?
Mseto ni sawa. Lakini sio kama huu ambao wanadai CUF wanaupendelea. Kama wapiga kura wamepiga kura kuchagua CCM kushikilia kiti cha Urais, na ukawa na Makamo mmoja (atakayetokea CUF), Mathalani Rais amefariki katika kipindi cha chini ya miezi sita baada ya kushika madaraka. Jee CUF (kwa maana ya Makamo wa Rais) apewe satuwa ya kushikilia Urais. Jee unawaaqmbia nini wapiga kura (walio wengi) ambao wamechagua CCM katika Urais kwa muhula huo wa miaka mitano? Wapi Demokrasia hapo?Patamu hapa kwa MAKAMU wa RAISI,CCM wanataka wawepo makamu wawili wa RAISI,na CUF wanataka makamu MMOJA tu,CCM wanataka inapotokea RAIS hayupo kwa njia yoyote ile,basi makamu wa PILI wa raisi ndio akaimu kiti,CUF wanataka awepo MAKAMU MMOJA tu(ambao wanategemea wataikamata nafasi hiyo) basi akaimu nafasi hiyo mara moja,mnasemaje hapa,ingawa hesabu ya CCM siielewi kabisa.
Anzisheni hiyo serikali kwa faida yenu na vizazi vijavyo, huku bara wapinzani wnaenda kwenye uchaguzi wakijua wanashindwa na wakipata hizo kura ndogo hawaingii serikali eti mambo taratibu taratibu!!
Mkiishaanzisha hiyo serikali mkae pamoja muangalie jinsi ya kupeana talaka na Tanganyika.
Be careful mkikosana hatutaki wakimbizi huku!
Kwa hiyo wanaombwa kuridhia maridhiano ambayo hata hawayajui?? Nafikiri ni muda muuafaka kuwaita Karume na Seif waje waeleze hayo maridhiano yao. nafikiri Karume na seif walitaka kuwatega wawakilishi ila janja inastukiwa. Can't wait for the CC on Sat and NEC on Mon.
.
Shamhuna always anasmile, ameshaambia he is next, na siasa za ZnZ ni fitna sana, huku akifurahi na kujipa moyo kumbe kila mmoja kaambiwe ni yeye, Huku Khatib akisubiri, Dr. Mwinyi akiamini uraisi ni haki ya watoto wa maraisi kama alivyo Balozi Karume. Naye Nahodha ndiye wa pili wa Karume anajua ndiye yeye. Dr. Bilal baada ya kufanyiwa mtimanyongo mara mbili, hii kwake ndio last chance basi tuu huku mambo si mambo, ilimradi.
"4. Baraza lifanye marekebisho ya vifungu vya 39, 42 na 62 ili kuweka utaratibu wa serikali ya Umoja wa kitaifa."
Kwa faida a yote hivi vifungu vina semaje haswa? Ili wote tujue ni nini haswa kina taka kufanyiwa marekebisho.
Mzee Mwanakijiji, hata mimi mwanzo nilidhani hivyo kuwa CCM itakataa kuanzishwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, ila mood niliyoiona humu, CCM, CUF lao moja, Baraza litaridhia uanzwishaji wa serikali hii ya umoja wa kitaifa ila litaweka referendum as a precondition.
Hawa CCM wajajanja hapo kwenye referundum ndiyo mchezo ulipo. Hivi sasa wanajaribu kutuliza mambo wewe subiri CUF wakubali kuwa serikali ya umoja wa kitaifa ije baada ya uchaguzi then baada ya uchaguzi utasikia kilio.