Acha nijaribu kujibu maswali matatu hapo juu:
1. Ikitokea uchaguzi ukazuiwa, ndiyo mwanzo wa kufanikiwa kwa ajenda husika (No Election) na kitakachofuata ni kufanya mabadiliko ya kisheria, kanuni na mifumo ya uchaguzi (Reforms). Rais ataitisha Bunge (wabunge wa zamani) na Bunge hilo litapitisha sheria ya kuongeza muda madarakani kwa serikali iliyopo, kisha hatua zingine za kutunga sheria, kanuni na marekebisho ya mifumo ya uchaguzi zitaendelea.
2. Kama hatua namba 1 ikifanikiwa hapo juu, siyo CCM wala vyama pinzani vitakuwa na pingamizi. Sote kama Taifa tutapaswa kutembea kwa mdundo huo huo wa mabadiliko.
3. Ikitokea baadhi ya wananchi na baadhi ya vyama na pengine nguvu kubwa ikatumika kufanya uchaguzi, kutatokea mgawanyiko mkubwa kama Taifa, na tutaweka historia ya kuwa na uchaguzi wa hovyo kuliko ule wa 2020. Uchaguzi unaweza kususiwa hata na Waangalizi wa ndani na wa nje (wa kimataifa). Ushiriki wa wananchi kupiga kura unaweza kuwa hafifu na kusababisha matokeo kupikwa ili kutimiza lengo. Hatua hizi huchafua sura ya nchi kimataifa na pengine kutotambuliwa kwa ushindi huo.
'Tunahitaji Amani : kabla, wakati na baada ya Uchaguzi'