No reform no election's

No reform no election's

lutemi

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2013
Posts
1,748
Reaction score
1,388
MHESHIMIWA RAIS MUNGU AKIKUPA NAFASI HUWA HAIJIRUDII MARA MBILI na KUMBUKA kwamba anataka wakati wote utumie uta wala wako kwa hekima.

1. Ipe ZANZIBAR UHURU KAMILI kwa kuandika KATIBA ambayo uliisimamia (Zanzibar una wajukuu zako, una makaburi ya ndugu zako, Mila na desturi zote zipo ZANZIBAR) hata kama utaacha kuna siku hutakuwa RAIS na atakuja mwingine ambae atarekebisha na hata pengine Mali ulizo nazo bara zikataifishwa hatuombei na ukajutia kwanini hukuweka misingi imara.

2. Muite mwenyekiti wa chadema hata kama ana maneno usiyoyapenda lakini tafakari mandiki yake ina nini ndani yake kabla waliolala hawajaamka. Unajua kila mtawala ana watu wanaompenda na wasio mpenda chunguza wasio kupenda wananguvu kiasi gani . Hawa wanaweza wakashirikiana kudraft barua na mwisho wakapita kwa wahisani na nchi ikapitia wakati mgumu Sana. Usichukulie jambo hili kuwa rahisi Sana .

3. MHESHIMIWA RAIS hivi akiwaeleza mabalozi kwa takwimu ya watu waliokufa kwaajili ya uchaguzi au matumizi ya misaada inavyofujwa unadhani nani Ataadhirika?

4. Faida ya no reform no election's ni hii
Unaweka misingi ya kiutawala halali kwa nchi iliyopiganiwa kwa muda mwingi
Mapungufu ya muungano yatakuwa yametatuliwa kwa asilimia Mia moja
Watu watachangia mawazo wakati kukiwa na Amani

Umepewa kutawala hata miaka miwili zaidi kuandaa kilicho Bora zaidi tume ya UCHAGUZI, KATIBA mpya.
Mwisho utakumbukwa milele.

Katika swaumu hii ikupe Tafakari ya kina utengeneze nchi sio kuziba viraka.
 
Kwa mtanzania yeyote mwenye mapenzi mema, ataunga mkono juhudi za kutengeneza katiba mpya.
Amani na usalama wa Taida letu ni zaidi ya maslahi ya kichama na madaraka.
Amina.
 
Tufanye yote, tuseme yote, tudai haki zote lakini tupambane wenyewe tusiwategemee hao wanaoitwa " wahisani" . Hao wahisani ndio wanaofadhili mauaji ya ndugu zetu pale Kongo. Hao wahisani ndio wanawafadhili Boko Haram kule Nigeria. Nchi yetu itapambaniwa na kukombolewa na SISI WENYEWE. Hata hao wahisani wakiwa wenyewe wanashangaa imekuwaje karibia majirani wetu wote wametwangana sisi hatujawahi. Wanatamani na sisi tuonje ladha ya ukimbizi. Tafadhali, kupambania taifa letu ni jukumu letu na hao wahisani ambao kiuhalisia ni wauaji hawawezi kutusaisia kwanza hawatupendi pili hawatoi kitu bure. Kama mzungu mwenzao Zelensky wanamkaba koo atapike pesa jiulize sisi watatufanya nini. Tuache utegemezi, tujipambanie.
 
Back
Top Bottom