No reforms No election ni project nzuri lakini ngumu mno. Plan B & C ni ipi?

Naona mnaanza kuchanganyikiwa.

Civil war? Yani niache kutafuta ugali familia yangu nikapigane vita ili chadema iingie madarakani?
Option yenye uhalisia ni chadema kushiriki uchaguzi.
Uzuri wanasema vita haina macho, huko unakotaftia ugali pakigeuka uwanja wa mapambano akili yako itafunguka tu. Hii kitaalamu inaitwa ā€œKUJIONGEZAā€. Mtaji mbio!

Machafuko yaliyotokea Magomeni Mwembechai mwaka 1998 yalidhihirisha kuwa Civil war is real na inawezekana kabisa. Hata wale watafutaji ugali hawakuonekana mitaa ile.
 
Tatizo ni viongozi wa CHADEMA kuwa na uchu wa madaraka. Viongozi wao bado wanavizia mkono ukatike kama ile hadithi ya fisi!.
Tuliisha shauri tangu mwanzo kuwa CHADEMA Kama chama kikuu cha upinzani wasishiriki uchaguzi wowote unaofuata baada ya kupata uzoefu wa uchafuzi wa 2019/20 kwa sababu CCM watafanya yao ili washinde, CHADEMA kwa mshangao mkubwa wakashiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu ambao umekuja kuthibitisha kuwa hawawezi kushinda kamwe kwa mtindo huu.

Sisi wengine tuliishatangaza kutokwenda kupiga kura hadi kuwe na meaningful reforms na mara zote tunaangushwa na hao hao CHADEMA ambao kama chama kikuu cha upinzani bado hawaamini kuwa wakisimamia kidete hoja yao ya No reforms no election watafanikiwa... Badala yake wameanza kugwaya vyama vidogo vidogo visivyo na ushawishi eti wao wakishiriki uchaguzi utakuwa crƩdible..... Hapana!!!

CHADEMA msishiriki uchaguzi huu wa 2025 kama hakuna reforms, nyie jikiteni kwenye hoja ya Reforms na katiba mpya kama tulivyodai uhuru ...CCM safari hii hawataweza kujitangazia ushindi mahali penye ushahidi wa uchafuzi na hila....Huo ndio ukweli unaowatisha watawala sasa hivi.
 
Naona mnaanza kuchanganyikiwa.

Civil war? Yani niache kutafuta ugali familia yangu nikapigane vita ili chadema iingie madarakani?
Option yenye uhalisia ni chadema kushiriki uchaguzi.
Nafikiri haujui unachosema hapa.

Hivi kwa historia ya Tanzania, kuna mikoa iliyokuwa na utulivu na 'amani' iliyopitiliza Kama mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara?
Wewe katika maisha yako hapa Tanzania, Je, uliwahi kufikiri au kutarajia kwamba Mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara ingeweza kukumbwa na Vurugu kubwa sana kiasi kile wakati ule wa Vurugu za Gesi zilizotokea huko kwenye mikoa hiyo?

Wewe ulitarajia kwamba mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara ingeweza kulipuka kwa vurugu kama vile ilivyotokea huko??

Ukichunguza kwa umakini Sana utagundua kwamba Watu/Wananchi wengi Sana hapa nchini wanafahamu kuwa kuna baadhi ya maeneo au mikoa fulani fulani hivi kama vile Tarime-Mara, Arusha, au Mbeya ndio maeneo yenye Watu ambao ni watata, ambao wanaweza kuanzisha vurugu kiurahisi muda wowote ule. Lakini kumbe kiuhalisia hali ipo tofaufi kabisa na fikra hizi za Watu wengi, Lindi na Mtwara zilithibitisha kuhusu suala hili kupitia zile Vurugu za Gesi.
 
Ccm haiaminiki tena hakuna kukaa chini na ccm, njia ya no reforms no election ni njia bora na sahihi, baadae kidogo itaeleweka na italeta impacts kuwa na subira.

Lisu anawajua vizuri ccm huwezi kukaa na ccm mkazungumza kuhusu chaguzi na wakakuelewa watakuhadaa tu.
 
Sema mbowe sio chadema
 
Huu ujumbe wa no reform, no election inabidi uwekwe kuonyesha jinsi unavyogusa moja kwa moja na kuchangia umaskini na ugumu wa maisha ya kila siku kwa Watanzania wengi.

Kwamba, ufisadi, rushwa, ukosefu wa maji, umeme, huduma za afya, elimu, miundombinu ipo hivyo sababu watawala hajali maslahi ya wananchi wala hawategemei kura zao au kuwajibishwa na wananchi.

Bila mabadiliko, hakuna chaguzi imekaa kisiasa zaidi, utaeleweka kwa watu wanaofuatilia siasa ila sio wananchi wengi hasa vijijini.
 
Nikweli na mambo yalikuaja kuwa moto pale ilipozaliwa ukawa, ila ccm wakaingia mzigoni wakawatawanyisha lipumba na dr Slaa na ikumbukwe walikua na nguvu ndani ya ukawa, ule umoja ule ungeenda mpaka mwisho wa uchaguzi , kingekua ni kivumbi japo ujio wa lowassa pia ilikua ni kivumbi
 
Hatakuelewa
 
Naona mnaanza kuchanganyikiwa.

Civil war? Yani niache kutafuta ugali familia yangu nikapigane vita ili chadema iingie madarakani?
Option yenye uhalisia ni chadema kushiriki uchaguzi.
Ishu sio chadema ishu ni wananchi kuchagua kiongozi wanaemuona anafaa na sio kuchaguliwa na jeshi la polisi
 
Hii Civil War ndii Plan D.
########
Mathalan marekebisho yatatokea, tena yatokee kwa kukubalika na masuala yote tunayotaka wana CHADEMA, na vyama vingine vya upinzani, yaani sheria za uchaguzi, katiba mpya, tume ya uchaguzi kadha wa kadha?

Je, tutakuwa tayari kuingia Uchaguzi ikiwa bado ni miezi michache sana imebakia kufanya kampeni?

Tuna sera gani za kuwauzia wananchi?
 
Hatujasema bila Reforms tutasusia, tumesema bila reforms tutahakikisha Uchaguzi haufanyiki kabisa.
 
Sera zipi utakazouza na baada ya kuuza hizo sera unategemea nini kama CCM tayari washajipa ushindi🤣?

Yani ni sawa na kushindana mbio fupi na mwenzio aliyejifunga maboya halafu wewe kwa hila umefungwa matofali miguuni. Ni wazi kuwa atakushinda mbio tu sababu hamna Fairness. Kinachopiganiwa hapo ni fairplay, kama maboya basi wote mfungwe maboya sio mmoja amefunga tofali mwengine boya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…