Nobel na Mo Ibrahim zanukia kwa Kenyatta

Nobel na Mo Ibrahim zanukia kwa Kenyatta

Kenyatta bado ni shujaa wa demokrasia Africa, hata Marais wenzake wa Africa wanamshangaa kukubali kwake kuiachia mahakama mshike masharubu kiasi hiki huku akiwa Amirijeshi mkuu wa Kenya. Kitu kama hicho ni nadra kutokea kwenye nchi nyingine za Africa.
Wewe ndo hujui historia ya kenya mpaka kufika hapo ilipo. Kwenda mahakamani ilikua ndo nia mbadala wa kuepusha ghasia zisitokee, angezuia mahakama kufanya kazi pangechimbika. Angekua ameridhika asingewaita majaji waliotoa hukumu kua ni wakora.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndo hujui historia ya kenya mpaka kufika hapo ilipo. Kwenda mahakamani ilikua ndo nia mbadala wa kuepusha ghasia zisitokee, angezuia mahakama kufanya kazi pangechimbika. Angekua ameridhika asingewaita majaji waliotoa hukumu kua ni wakora.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aaa suala la machafuko na kupoteza maisha ya wananchi sio jambo kubwa sana linaloogopwa na viongozi wa Afrika. Mbona Burundi, DRC, Rwanda, Uganda, Sudani Kusini, Sudani, Comoro na kwingineko Afrika damu zilimwagika na bado zinamwagika hadi leo ili kupata urais au kuendelea kubaki madarakani?

Hakuna ubishi kuwa Kenyatta anastahiki heshima ya pekee mpaka hapo alipofikia. Angetaka angesalia madarakani kwa kutumia jeshi, polisi, na usalama wa taifa kukamata jaji mkuu na wadau wengine wengi wanaomkera kama vile wanavyofanya viongozi wa nchi nyingine (akina Yahaya Jemi, Bagbo, Kirr, Kabila, Nkuruzinza, Misri, nk)
 
Mwanzoni alidhani wasingebatilisha matokeo lakini ndio maana akawaachia. Ila sasa hivi ameshabadilika na jana alisema kua majaji wakivaa magauni wanajiona wana akili kuliko wakenya wote

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado ndiye Amirijeshi Mkuu wa Kenya, kama akitaka hata leo anaweza kukatalia madarakani kama wanavyofanya wengine. Lazima tukubali kuwa Kenyatta sio kama wengine Afrika. Huu ni mwendelezo tu wa busara zake, kumbuka kuwa Hata wakati wa uongozi wake wapinzani wake walikuwa huru kusema na kufanya mikutano yao bila bughudha kitu ambacho ni marufuku kwa mataifa mengine..
 
Nobel kwa wizi wa kura? Mimi nadhan Jaji Mkuu ndie anaestahil hiyo tuzo kwa kuhakiki haki iliyokua imeporwa na wez inatendeka

Sent using Jamii Forums mobile app

Kura hazikuibiwa ila processes zilikuwa na makosa, mfano forms hazikujazwa zile original, lakini majaji wangekubali kura zilizokuwa katika vituo kuhesabiwa upya bado ingejulikana kuwa Uhuru alishinda. Lakini yote hayo yametokea kwa sababu maalum ili mshindi apatikane na kura nyingi zaidi za ushindi.
 
Back
Top Bottom