Bandari ni jambo la muungano.
(Pamoja na usafiri wa anga, posta na mawasiliano ya simu).
Lakini Zanzibar walianzisha mamlaka yao ya bandari, sijui kwa utaratibu upi maana katiba inasema wazi ni jambo la muungano.
Muungano wetu umejaa uhuni uhuni mwingi, na siku zinavyozidi kwenda Zanzibar wanazidi kuanzisha taasisi zao kwa mambo yanayopaswa kuwa ya muungano, wakati huohuo vya Tanganyika wanavitaka pia.