kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Timu zetu zote hazifanyi vizuri na hazijawahi kufanya vizuri miaka ya usoni. Kumtimua kocha huyu ni sawa na kuficha nyuso za watendaji wa mpira nchini ndani ya track-suit ya kocha. Kocha hachezi na wala haruhusiwi kuwapanga akina Okwi, Niyozima, Twite, Tabwe, Cotinho, n.k. Tanzania hakuna vipaji vilivyotengenezwa kucheza mpira ndo maana hata vilabu vinaomba visajili wachezaji 10 wa kigeni kwenye vilabu vyao. Tuache kucheza mpira wa kimataifa kwanza tuandae timu zetu. Kumfukuza Nooij kwasababu ya timu ya taifa kufungwa ni kumharibia CV kocha wa watu. Tatizo hapa ni vuruvuru ya TFF na serikali kwenye mpira. Ni heri hata ya akina Ndolanga kuliko hawa waliojigamba kuwa ni watu wa mpira. Mwacheni Nooij tujilaumu wenyewe na wachezaji wetu.