NOOIJ ni kama wenzake tu

NOOIJ ni kama wenzake tu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Timu zetu zote hazifanyi vizuri na hazijawahi kufanya vizuri miaka ya usoni. Kumtimua kocha huyu ni sawa na kuficha nyuso za watendaji wa mpira nchini ndani ya track-suit ya kocha. Kocha hachezi na wala haruhusiwi kuwapanga akina Okwi, Niyozima, Twite, Tabwe, Cotinho, n.k. Tanzania hakuna vipaji vilivyotengenezwa kucheza mpira ndo maana hata vilabu vinaomba visajili wachezaji 10 wa kigeni kwenye vilabu vyao. Tuache kucheza mpira wa kimataifa kwanza tuandae timu zetu. Kumfukuza Nooij kwasababu ya timu ya taifa kufungwa ni kumharibia CV kocha wa watu. Tatizo hapa ni vuruvuru ya TFF na serikali kwenye mpira. Ni heri hata ya akina Ndolanga kuliko hawa waliojigamba kuwa ni watu wa mpira. Mwacheni Nooij tujilaumu wenyewe na wachezaji wetu.
 
you are right man,tunashindwaje kuunda timu ya pili ya taifa iwe chini ya makocha wazando? mwanbusi ,shime ,mkwasa tunao watu kibao lakini timu inachaguliwa wiki moja kabla ya mashindano kweli tutaweza?.wachezaji wanachaguliwa kuunda taifa stars hata namba kwenye timu zao hawana .....nacheeekaaaaaa.
 
Rekodi zinaonesha katika mechi 5 za mwisho kabla ya Nooij hajatimuliwa, Taifa Starz ilifungwa zote.
 
you are right man,tunashindwaje kuunda timu ya pili ya taifa iwe chini ya makocha wazando? mwanbusi ,shime ,mkwasa tunao watu kibao lakini timu inachaguliwa wiki moja kabla ya mashindano kweli tutaweza?.wachezaji wanachaguliwa kuunda taifa stars hata namba kwenye timu zao hawana .....nacheeekaaaaaa.

Ni yule mwendawazimu tu atakayekubaliana na TFF kumtimua kocha kwasababu timu hii ya taifa haikufanya vizuri, zilizopita nazo je! badala ya kumtimua Malinzi na CCM inayoiandalia serikali yake ilani ya kutekeleza mnatimua makocha, kwa kosa lipi.
 
Back
Top Bottom