Noti mpya hazina ubora?

Noti mpya hazina ubora?

wao raia wanasema hazina kiwango sasa unafikiri beno ndulu afanye nini? mi naona watueleze kwanini wametengeneza hizo noti mpya na jingine kwanini wanazichanganya na noti za zamani..
 
Wana JF.
Kimuonekano, Noti Hizi mpya zinaondolewa kwenye Mzunguko.
Si matarajio yangu, kwnda Benki na kupewa Noti za zamani ilhali hizi noti zilitakiwa kutolewa katika mzunguko kupisha uingizaji wa noti mpya.

Jinsi mambo yanvyoeenda si muda mrefu hizi noti mpya zitaondoka kabisa katika Mzunguko.

Je? Si haki yetu watanzania kujua Kinachoendelea hapa? Kama sio ufisadi kwanini hili jambo linafanywa kisirisiri?

Nini kinaendelea hapa?
Juma lililopita nilipitia barabara ya kilwa nikakutana na gari la Polisi likiendeshwa Hovyo Hovyokutokea bandarini likitaka tupishe njia Huku likifuatiwa na Maroli 7-8 yamebeba makasha makubwa ya futi 20 hivi yakisindikizwa chini ya ulinzi mkali wa polisi na wanausalama toka Benki kuu yenye namba za SU.wadadisi wakasema hayo malori yamebeba pesa!kwahiyo nafikiri labda wameleta mbadala wa zile za mwanzo!
 
Juma lililopita nilipitia barabara ya kilwa nikakutana na gari la Polisi likiendeshwa Hovyo Hovyokutokea bandarini likitaka tupishe njia Huku likifuatiwa na Maroli 7-8 yamebeba makasha makubwa ya futi 20 hivi yakisindikizwa chini ya ulinzi mkali wa polisi na wanausalama toka Benki kuu yenye namba za SU.wadadisi wakasema hayo malori yamebeba pesa!kwahiyo nafikiri labda wameleta mbadala wa zile za mwanzo!

jamani nimekwenda Bank jana nimedroo laki na nusu note za elfu kumi nikapewa noti 14 noti za zamani 1 mpya hii ni AIBU KWA SERIKALI YA CCM
 
Kula tano kwanza, its like u've been reading my mind. Jana nlitaka post hii thread....... kazi zikanizidi na uchovu nikashindwa post....

Nami nashangaa sana........ Mbwembwe zilizotumika na Governor ktk kuzinadi zilikua ni nyingi sana.......... Alianzia kwa Raisi hadi vyombo vya habari... Watu wakaanza zitumia, na ikagundulika zina makosa mengi mojawapo ni kutoa rangi, akalitolea ufafanuzi, kwamba haiwezekani eti ni za quality ya juu sana. Wataalam wa fedha watujuze, fedha mpya kuondoa zilizopo kwenye mzunguko inabidi zichukue muda gani? Maana muda umeenda sana, na badala ya fedha mpya kuongezeka zinapungua. Je, wanataka tuambie kwamba 10% ilitumika hivyo fedha imekuja isiyo na viwango, kwa gharama zetu watanzania wanazitoa na kwenda chapa zingine? Je, uchumi wetu uko hoi bin taaban, japo Governor Ndulu, JK na Mkullo wanajitapa unakua ilhali asilimia za ukuaji wao zinatofautiana hivyo zililetwa kuongeza fedha kwenye circulation? Maswali ni mengi kuliko majibu, we really majibu tena kwa mbwembwe zile zile na ufafanuzi ule ule wa NOTI MPYA HALALI KWA MALIPO YA SHILINGI.............
 
Jamani noti mpya zipo na hakuna mpango wa kuziondoa kama wengi mnavyofikiri, hazitolewi kwa kasi kana kwamba hizi za zamani zinatakiwa kupotea ndani ya mwezi, kama ni hivyo tungepewa muda wa kwenda kuzibadilisha benki kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.Hakuna uharaka huo zitajiondoa taratibu na hizi mpya zitakuwa nyingi kwenye mzunguko taratibu.!!!!
 
Kwa jinsi zilivyokosa ubora watakuwa wamefanya la maana sana kuziondoa
 
Huo ni ufisadi uliokomaa wakuu, habari nilizonazo kuhusu note mpya zilitolewa kwa sababu ya noti za zamani kutumika sana kwenye uchaguzi uliopita hivyo benki kuu ikapungukiwa mshiko, sululisho ikawa ni kuchapisha noti mpya.
 
hiyo ndo serikali ya ****** mnategemea nini kama sio ubabaishaji ulikithiri??? waliona watu wanalalamikia ubora wake hasa zilipoonekana kuchafua na kustain nguo zikiwekwa mifukoni, wakasema ndiyo noti original.. sasa wameshtuka wameingia mkenge noti mbaya wanaziondoa kimya kimya.. Mkuu wa kaya sijui anasemaje manake wakati zinaingia sokoni walizitangaza kila mara na kusifia ubora wake..kweli nchi inakwenda pabaya...
 
kwa kumbukumbu zangu mbovu ilikuwa baada ya kutengenezwa note/pesa mpya basi kiliwekwa kipindi maalumu cha kuhakikisha pesa hizo hazipo mikononi mwa raia na watu walitii kwa kuzipeleka kwenye mabenki... lakini pesa za sasa me hata sijawaaelewa eti zitaendelea kutumika na zile za zamani!! naona kama inachanganya vile au kwa sababu ni mabadiliko makubwa ya pesa (mabadiliko yaliyohusisha kubadilisha noti zote)???
 
Jamani noti mpya zipo na hakuna mpango wa kuziondoa kama wengi mnavyofikiri, hazitolewi kwa kasi kana kwamba hizi za zamani zinatakiwa kupotea ndani ya mwezi, kama ni hivyo tungepewa muda wa kwenda kuzibadilisha benki kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.Hakuna uharaka huo zitajiondoa taratibu na hizi mpya zitakuwa nyingi kwenye mzunguko taratibu.!!!!

Kapuni, kinachoonekana ni kwua awali noti mpya zilikwua nyingi lakini zinaanza kupungua taratibu... kama trend ikiendeleas hivi kuna hatari zitatoweka kabisa baada ya muda si mrefu. Kama kampeni ni kuingiza nopti mpya, tulitarajia kuwa za zamani ndio ziwe zinapungua, si hizo mpya
 
Tulishuhudia mbwembwe za Gavana na JK wakizindua noti mpya mwishoni mwa disemba 2010 na kutujuza kuwa Jan 2011 noti mpya tayari zitakuwa kwenye mabenki,WaJF NAOMBA mnijuze kunanini mpaka leo takribani miez sita kila noti zipo mbilimbili,why??
 
Tena sio hivyo tu, juzi nimeona noti za zamani mpya kabisa, inaonekana wanatoa zote. Nahisi muda si mrefu kuna bomu litalipuka, there is something fishy here. Kwa nini zitolewe zote?
 
mi nimesikia tetesi kua BOT wanazikusanya noti mpya kuzitoa kwenye mzunguko mana walizichakachua sana,we jiulize 'kizuri chajiuza kibaya chajitembeza' hizi noti mpya zinapigiwa promo sana kwenye media wakitaka tuamini nhigh quality ila ni MBOVU na hivi karibuni utaskia slaa kawadaka wachakachuaji BOT
 
Kwani hamjasikia kuna pesa feki nyingi kwenye mzungo ambazo zinaathiri uchumi wetu?
 
Kwani hamjasikia kuna pesa feki nyingi kwenye mzungo ambazo zinaathiri uchumi wetu?

Tatizo linabakia palepale...kwamba kiwango duni cha fedha kumeleta mianya kwa watu kutengeneza duplicate black money na zikaingizwa kwenye mzunguko,zingekuwa na viwango imara usingesikia mambo ya ''pesa feki''.
 
jamani nyie acheni tu, mie sasa hivi nimetoka kuvuta noti za zamani kwenye ATM, halafu juzi kwa macho yangu nilikuwa azania benki nikaona jamaa wa back desk anazipanga noti za zamani zikiwa mpyaaaaaaaa tena mafundo mafundo, niliguna tu na kujisemea moyoni tunaenda wapi Tanzania.

Walituambia hela mpya inayofiti kwenye wallet maajabu waleti yangu nikiziweka utadhani hazimo hasa kile cha miatano.
 
Back
Top Bottom