Noti Mpya ya Kenya: Wanaoficha hela chini ya kitanda!

Noti Mpya ya Kenya: Wanaoficha hela chini ya kitanda!

Kafrican

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2015
Posts
7,251
Reaction score
7,037
Baada ya banki kuu kuleta shilingi mpya za kenya ambazo hazina picha ya Rais yeyote, Hatimaye jana walizindua noti mpya za Kenya , mimi mwenyew sijafurahishwa sana na vil zinakaa ni kama tu noti nishawahi ziona za nchi zengine , Alafu katiba inasema hizo noti hazifai ziwe na picha ya rais yeyote, wametoa picha za ma rais upande wa mbele na kueka wanyama, lakini upande wa nyuma bado wamebakisha picha ya KICC ambayo iko na sanamu ya Kenyatta. technically sanamu si picha lakini hapa naona kesi ikienda mahakamani na CBK wakilazimishwa kurudi kuchora upya hizo noti jambo ambalo litasababisha kodi zetu kutumika kiholela manake kampuni ya kuchapisha itakua ilishalipwa kuanza kuchapisha hizi noti zenye KICC.

Anyway, tukirudi kwa mada, Wale ambao wanapenda kuficha hela walizoiba chini ya kitanda, muko na mpaka Oct mwaka huu kupeleka hizo hela benki mkageuziwe na hela mpya, kumbuka ukienda benki na hela nyingi ni lazima ueleze chanzo cha mapato yako.....

1115113

D7-GK9bXUAEB18g.jpg

D7-HZuyWsAAadHu.jpg

D7-HZu0XoAU4jjy.jpg

D7-HZuxXYAEq3Vg.jpg
 
Attachments

  • 1559470140247.png
    1559470140247.png
    12.9 KB · Views: 44
Kati ya marais wote ambao walifaa kuwa kwenye noti hizi Emillio Mwai Kibaki alistahili, tena sana. Ila naona Mzee Jomo Kenyatta amebadilisha pozishen akaketi labda akishachoka atalala ampishe Obako. [emoji1]
Hahaa nakuunga mkono. Rais mmoja tu ndio anastahili sifa na pongezi na nafasi kwenye noti, Emilio Mwai Kibaki.
 
Kwa bongo hao wanaoficha fedha nyingi ndani tunasema "imekula kwao"
 
kwa hio wapeleke za zamani wageuziwe na mpya sio?? basi sawa!!
 
Njooni mfundishwe kiswahili.. tafsiri ya feel siyo gusa..

feel/hisi
touch/gusa
TOUCH = to move especially the hand or another part of the body lightly onto and off something or someone.
eg 1. The paint is wet - don't touch (it),
eg 2. He touched the girl on the arm to get her attention.
eg 3. The child touched the worm with a twig.

FEEL = to touch something in order to discover something about it.
eg 1. Just feel how cold my hands are!
eg 2. He gently felt the softness of the baby's cheek.
eg 3. I was feeling in my bag for the keys.

Mbona iko sawa mkuu?
 
Kiaina nina wasiwasi na hili agizo, nahisi hela zitatoweka mtaani maana hizo noti walizozitia kweye magodoro ndizo huwa wanatumia tumia huku kitaa kununua nunua, naomba msaada wa wachumi watusaidie kutabanaisha hili.
 
Mimi ni mchumi lakini hili sio eneo langu la expertise, mambo ya money and banking hio nilisoma tu kwa shule. Lakini kulingana na watu, inasemekana kuna mabilionea kama Wahindi na former civil servants ambao wameweka pesa ndani ya nyumba ili kuzuia kulipa ushuru au kuzuia maswali ya pesa ilikotoka. Hii imefanya pesa ikose kucirculate ndani ya uchumi, na kupunguza ukuaji wa uchumi. Kwa hivyo hio pesa waliyoficha watalazimika kuirudisha ndani ya uchumi ndani ya miezi minne, hio itasaidia kuboost money supply expansion and circulation in the economy. Wakati Kwa mfano unaeza gundua a former civil servant ambaye alikuwa na mshahara wa elfu arubaini kila mwezi akiwa na pesa yenye thamani ya milioni mia moja. Huyo mtu hawezi peleka hio pesa kwa bank, ataificha. Lakini kwa maoni yangu hatuwezi fahamu effect itakuwa ipi kwenye uchumi hadi baada ya miezi au miaka kadhaa. La mwisho, hili jambo litapigana na ufisadi kwa kiasi fulani. Kwa maoni yangu mimi naikubali kwa sasa na pia sijasikia wachumi mashuhuri wakiipinga kama akina Ndii au Kwame Owino.
 
Asante kwa jibu lako bro, ila bado nina wasiwasi
- Kwamba hili agizo litasababisha mafisadi waweweseke, hilo halina ubishi maana lazima wawaze wapi pa kupeleka mamilioni yao.
- Hela kurudishwa kwenye benki, zitachochea mzunguko wake mtaani, hilo pia ni jambo chanya

Sasa wasiwasi wangu uko kwa wale wenye hela ambazo wamezifukia na hawawezi kuzirudisha kwenye mabenki kisa walizipata kwa njia za kifisadi, hizi hela wao wamekua wakizitumia tumia kununua nunua hapa na pale, sasa hawataweza kuzirudisha na zitabaki huko huko bila thamani.
Huoni hapa tutakua tumepoteza kiaina, mamilioni yaliyofukiwa na hayana thamani, au labda watumie muda huu kununua mali kwa njia ya pesa taslimu tena kwa mkurupuko.
 
Ndio una point hapo. Kuna watu ambao watashindwa kurejesha hio pesa ndani ya uchumi na huenda ikapotea hivyo. Wanasemanga, hakuna jambo nzuri linalokosa ubaya wake. Hio kupoteza pesa kwenye uchumi ilifanyika India hivi majuzi walipobadilisha noti zao. Lakini hilo tatizo ni temporary kwa sababu kazi ya central bank ni kuprint pesa ikiwa kuna shortage kwa hivyo India waliprint pesa na kuondoa huo uhaba. Kenya central bank pia inaweza print noti zaidi ikiwa kuna uhaba ila wasizidishe idadi za noti na kufanya thamani ya shilingi kuwa duni kama vile Iddi Amin alivyofanya. Nadhani itakuwa shortage temporary lakini kama tu India tutarekebisha huo uhaba.
 
Back
Top Bottom