LGE2024 Nov 27 Mapumziko ni Bara tu, Zanzibar ni siku ya kazi kama kawaida

LGE2024 Nov 27 Mapumziko ni Bara tu, Zanzibar ni siku ya kazi kama kawaida

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Wao wanafanya lini uchaguzi wa serikali za mtaa-?
 
Kwani Barua inasemaje...!? Au wameandika barua bila kufikiria kuwa Zanzibar ni Nchi...!!
 
Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU Zanzibar ambaye pia ni Msemaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hillary, amesema hakutokuwa na mapumziko Visiwani Zanzibar November 27 hivyo kazi zitatakiwa kuendelea kama kawaida.

Katika taarifa rasmi ya IKULU, Hillary amenukuliwa akisema “Novemba 27 mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ameshatangaza kwamba siku hiyo itakuwa siku ya mapumziko kuruhusu Wananchi wa Tanzania Bara kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kuchagua Viongozi wao wa Serikali za Mitaa”

“Kwavile Zanzibar hakuna uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawaarifu Wananchi wote Jumatano Novemba 27 2024 ni siku ya kazi kama kawaida Zanzibar, ahsanteni” ——— Charles Hillary. #MillardAyoUPDATES
 
Attachments

  • 1732542920320.jpg
    1732542920320.jpg
    281.1 KB · Views: 5
Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU Zanzibar ambaye pia ni Msemaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hillary, amesema hakutokuwa na mapumziko Visiwani Zanzibar November 27 hivyo kazi zitatakiwa kuendelea kama kawaida...
Zanzibar wana islamic new year day, nyie mnayo?
 
Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU Zanzibar ambaye pia ni Msemaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hillary, amesema hakutokuwa na mapumziko Visiwani Zanzibar November 27 hivyo kazi zitatakiwa kuendelea kama kawaida...
Watu wavivu wanapenda sana .mapumziko
 
Back
Top Bottom