Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU Zanzibar ambaye pia ni Msemaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hillary, amesema hakutokuwa na mapumziko Visiwani Zanzibar November 27 hivyo kazi zitatakiwa kuendelea kama kawaida.
Katika taarifa rasmi ya IKULU, Hillary amenukuliwa akisema “Novemba 27 mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ameshatangaza kwamba siku hiyo itakuwa siku ya mapumziko kuruhusu Wananchi wa Tanzania Bara kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kuchagua Viongozi wao wa Serikali za Mitaa”
“Kwavile Zanzibar hakuna uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawaarifu Wananchi wote Jumatano Novemba 27 2024 ni siku ya kazi kama kawaida Zanzibar, ahsanteni” ——— Charles Hillary. #MillardAyoUPDATES