November 25 yagombaniwa, Efm/TvE vs Clouds Media

November 25 yagombaniwa, Efm/TvE vs Clouds Media

Kama kumbukumbu zangu zitakuwa vizuri fiesta haikuwa brand ya clouds bali ilikuwa ya east Africa Kwa udhamini wa sigara ya sm na vanue yake ilikuwa daimond jubilee.

Ruksa kunisahihisha

Fiesta haijawahi kua ya East Aftica.. tangu inaitwa summer jam mpaka kua fiesta iko chini ya clouds
 
Kwanza kbla ya yote leo wametaja list ya wasanii watakaoimb fiesta,mr blue,vanesa mdee,jux,weusi,be pol,stamina,rma,ali kiba,maua sama, aslay,na bdo list inaendlea sasa swali show ya efm uend kumwangalia msanii gani mda mwngne tjiulize au ndo kna dula makabila,ishu so bure ishu unaenda kumwngalia nani wa maana
Usikariri...Kumbuka kuna Mwana FA na AY (wana ugomvi pamoja na kesi na Tigo) na kuna timu nzima ya WCB...Ongeza na wasanii waliokuwepo kwenye Tamasha la Muziki Mnene ambao ni Nay wa Mitego, Izzo Business, TID..Chemical, Ruby..Na wasanii wanaotamba na Singeli (kumbuka Dar Singeli ndio nyumbani)...
 
Kama kumbukumbu zangu zitakuwa vizuri fiesta haikuwa brand ya clouds bali ilikuwa ya east Africa Kwa udhamini wa sigara ya sm na vanue yake ilikuwa daimond jubilee.

Ruksa kunisahihisha
Fiesta ameimba R Kelly, hao clouds Tamasha lao lilikuwa linaitwa Summer Jam.
 
Walianza kutangaza Clouds kuwa Ruge atakua Live kwny vyombo vyao ndo hao TV E wakafuata..! Na hio tarehe 25 toka wiki iliyopita Clouds wanaimba kuwa Fiesta Dar wao wametangaza leo tamasha la bure tar 25 unahisi nani mchokozi?
Wewe ni mrithi wa Zamaradi?
 
Tve ni cmpetitor wa clouds, na tve akigangamala atampiga bao clouds.
Mpambano gani unaweka tamasha bure kama wanajiamini na wao waweke kiingilio hapo ndio tutaita Mpambano, Uo ndio umasikini waafrika wengi tumejaliwa..! Kufanikiwa kwa MTU , uwa inatuuma sana...! Wao wanaumia Sana'a wakiona jamaa anavyopiga hela na fiesta yake.!! MSIWE NA AKILI ZA KAA
 
Usikariri...Kumbuka kuna Mwana FA na AY (wana ugomvi pamoja na kesi na Tigo) na kuna timu nzima ya WCB...Ongeza na wasanii waliokuwepo kwenye Tamasha la Muziki Mnene ambao ni Nay wa Mitego, Izzo Business, TID..Chemical, Ruby..Na wasanii wanaotamba na Singeli (kumbuka Dar Singeli ndio nyumbani)...
Ngoja nimpe orodha ya wabongo fleva wenye uwezo wa kusepa na kijiji na Clouds imewaweka pembeni kwenye hilo Lifiesta lao,

Yupo Dully Sykes, Sir Nature, TID, and likes.
 
Hata kama ni Competition hicho wanachotaka kufanya Efm/TVE ni utoto sasa... Kwa style hii maendeleo nchi hii ngumu sana

Inajulikana Fiesta ni brand ya clouds kwa nini usipange ratiba zako tarehe nyingine kama unahamu ya kutupa tamasha la bure? To me that is so low and pathetic! Kama wao ndio walianza kutangaza tarehe basi clouds wasogeze mbele
Tunasema wanachokifanya Tve/ Radio ni fikira za kimasikini sana, na kama wanafikiri ndio ujanja, viongozi wote walio na wanao chekelea hicho kitu wote ni watoto...
 
Waache nao wameze dawa walizokuwa wanawamezesha wenzao, tena ikibidi aletwe msanii toka nje, na hata wakiahirisha na sisi tunaahirisha.

Kama namwona Makonda atakavyoamrisha Fiesta iishe saa 6 huku EFM ikikesha...

Tunazima kiki, tunawasha muziki.
Ndoto za kimasikini hizi...
 
Upande mmoja ukitaka ushinde watangaze kumleta jukwaani yule billionaire wa 900, Namaanisha Dr. Shika
 
Mpambano gani unaweka tamasha bure kama wanajiamini na wao waweke kiingilio hapo ndio tutaita Mpambano, Uo ndio umasikini waafrika wengi tumejaliwa..! Kufanikiwa kwa MTU , uwa inatuuma sana...! Wao wanaumia Sana'a wakiona jamaa anavyopiga hela na fiesta yake.!! MSIWE NA AKILI ZA KAA
Mkuu niambie wp kwenye muziki mnene wametoza kiingilio? Kila mkoa ilikuwa bure sasa kwann unawalazimisha sasa hv watoze pesa!
 
Yani niende kwenye tamasha la bure nirudi na ngeu???? kwa sisi wapenda burudani na starehe tunapendelea matamasha yenye viingilio tena ikiwezekana bei ikiwa kubwa mana ustaarabu unakuwepo, tunahangaika kutafuta pesa haipaswi kupata mateso wakati wa kuitumia.....wahenga wanasema "bure gharama"
Fiesta nayo sehemu ya ustaarabu chaaaa
 
Mkuu niambie wp kwenye muziki mnene wametoza kiingilio? Kila mkoa ilikuwa bure sasa kwann unawalazimisha sasa hv watoze pesa!
Haaaa haaaaa. ! Wangekuwa na mapafu wangefuata na huko mikoani.! Wawaulize eatv ! Chaliiii..... Tuende mbele turudi nyuma Mawingu in jeshi lililoshiba, mapungufu kila MTU anayo na utofauti. In my life toka 2000 mi ni clouds FM, Habari Radio One.
 
Tunasema wanachokifanya Tve/ Radio ni fikira za kimasikini sana, na kama wanafikiri ndio ujanja, viongozi wote walio na wanao chekelea hicho kitu wote ni watoto...
Kama unahisi wanachofanya EFM/TVE ni fikra za kimsakini utakuwa unachemka...

Mwaka 2013 Lady Jay Dee aliandaa show yake kubwa tu katika ukumbi wa Nyumbani Lounge- Namanga...Ruge na Clouds nao siku hiyohiyo wakaandaa show ya Mwana FA ukumbi wa Makumbusho - Posta kwa lengo la kumkomoa Jide...Hawakufanikiwa kuharibu show ya Jide kwa sababu Jide alipewa support na Profesa Jay, Sir Nature & Wanaume Halisi, Grace Matata, Langa Kileo, M 2 the P, Mr Sugu na Bantu group Band ya Mzee Kalala....Mwana FA yeye alisindikiwa na Mandojo na Domokaya (ambao walipelekwa na Clouds kwa sababu tu walikuwa na beef na Lady Jay dee), Dully Sykes na Kilimanjaro Band ‘wana Njenje’..

Pia kumbuka kwamba kuna kipindi Mr Sugu na Vinega waliandaa tamasha la Antivirus viwanja vya Posta Kijitonyama ...Ruge na Clouds nao wakaandaa lao Leaders...Kijitonyama palifurika na siku hiyo Mbowe, Lissu, Mdee na wabunge wengine wa Chadema walipanda jukwaani...

Iweje leo uwatuhumu Efm/Tve?

Btw; kwenye dunia hii ya soko huria na utandawazi kila mtu/kampuni ana uhuru wa kufanya jambo analoona linafaa mradi tu havunji sheria...Efm/Tve ni vituo ambavyo vinajitangaza katika soko la habari na burudani...Mkakati wanaotumia kujitangaza ni pamoja na kuandaa matamasha ya bure na kutoa zawadi kwa wananchi kwa lengo la kuwavuta wasikilize/kutazama vituo vyao..Angalia matamasha kama Mchizi wangu, Shika ndinga na Muziki mnene au utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwa moja njue ya studio na kukutana na wasikilizaji wao (NJE NDANI)...Udhamini wa BIKO, Coca Cola na Fast Jet unawapa jeuri ya kuyafanya haya matamasha bure....

Sasa hivi EFM wanarusha matangazo yao mikoa ya Dar, Pwani, Mtwara, Mwanza, Mbeya na Tanga wanapatikana na mikoa jirani na hiyo...Muitikio walioupata katika mikoa hiyo ni mkubwa kiasi cha kuwa tishio kwa Clouds ambao matamasha tyao wanatoza viingilio...Umati uliohudhuria uwanja wa Sokoine juzi kwenye tamasha la Muziki mnene ni mkubwa sana sana...

Efm/Tve ni tishio kwa Clouds FM/TV....Clouds inabidi walijue hilo na kujipanga kushindana katika strategies badala ya mafumbo ya Ruge na public sympathy...

Sorry kwa waraka mrefu...

Wakatabahu...

Bala.
 
Back
Top Bottom