Huu upepo wa No reform No election ni mkubwa na una nguvu umeshika kasi kwa wananchi. Hii ni "ideology" na ni ajenda ambayo wananchi wanaielewa kwa urahisi kutokana na yaliyoonekana kwenye chaguzi zilizopita na hususani uchaguzi wa 2024. Ninashauri Serikal8 yangu tukufu ifanye marekebisho ya msingi kwenye katiba kuhusiana na Tume ya uchaguzi na sheria zake angalau marekebisho madogo. mjadala huu umevuka kiwango cha udhibiti hakuna namna. Viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya kiserikali ndani na nje ya nchi yameshauri hivyo. Hii ni pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM ndani. Tusidharau kwa jeuri na mazoea. Mikutano ya Chadema imekuwa ni LITMUS TEST.