Nsekela aongoza harambee shule za Marian, Bagamoyo

Nsekela aongoza harambee shule za Marian, Bagamoyo

CRDB wamechukua maji kisimani, wakenda kumwaga baharini. Marian wanao uwezo wa kujenga shule vizuri kabisa bila shida. Hii michango ilitakiwa kwenda "Mwembe kiuno" sekondari, au shule ya msingi "sogea tukae".

By the way, sioni kama lengo la kuzianzisha hizi shule za Marian linatimizwa kwa sasa. Imekua kinyume chake!
Na ni shirika Holy Ghost father's la zamani na kubwa sana
 
Hivi hizi shule za Marian zinamilikiwa na huyo Fr. Bayo kupitia mgongo wa kanisa au ni kanisa kweli kwa 100%? Isijekuwa kuna umafia kwenye suala la umiliki.
Bayo anaendesha kama mali zake yeye. Na Bayo ni mwakilishi wa Holy Ghost Father's ( spiritans) ambalo ni shirika la mapadre,masister na watawa kutoka kanisa katoliki.Nilifanya kazi Marian boys kwa miaka miwili nikishirili kuianzisha na Hata uwanja wa mpira niliuchora Mimi na wanafunzi na tukasimika magoli Yale,wanasoma hapo ni wenye pesa .Watu wa Pwani wanaosomesha hapo ni wahamiaji na wenye pesa.Watoto wa wenyeji wapo Kayumba hapo Kerege,Zinga etc.
 
Hivi hizi shule za Marian zinamilikiwa na huyo Fr. Bayo kupitia mgongo wa kanisa au ni kanisa kweli kwa 100%? Isijekuwa kuna umafia kwenye suala la umiliki.
Sidhani km za kanisa 100%maana Kwa Sasa Yale maadili ya ukanisa kama Kifungilo ,St.Fransic hayapo
Kwanza ada kubwa Sasa hivi
Pili watoto wanapewa pesa wako huru kwenye matumizi mnoo pale shuleni

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Bayo anaendesha kambmal zake yeye. Na Bayo ni mwakilishi wa Holy Ghost Father's ( spiritans) ambalo ni shirika la mapadre,masister na watawa kutoka kanisa katoliki.
Ni matajiri sana hawa jamaa. Hata huko kukusanya michango ni geresha tu waonekane hawana uwezo. Kuna kitu wanaficha.
 
Nimekumbuka kuna kanisa linamiliki shule ya msingi iliyojengwa kwa michango ya waumini, wakatakiwa kuweka paving na kununua bus la shule. Waumini wakawa wanalalamika kuwa wanatoa michango wakati shule inaendeshwa kwa ada kubwa na bado hata wao walio wengi hawawezi somesha watoto wao hapo!! Sasa sijui pesa zinakwenda wapi🤷

Hii nchi ufisadi kila kona.
 
"Sekondari ya Wasichana Marian ilijengwa Februari 1997 ili kuwapa fursa wasichana wa Mkoa wa Pwani na maeneo jirani kupata elimu bora"
Hivi hata viongozi wa dini siku hizi ni matapeli,hii shule lini ililenga kusaidia wasichana wa mkoa wa pwani?? Hata tukifanya sensa ndogo hapo sidhani kama wasichan wa pwani watafika hata 1%,
Mmmhhh!!!Nnaowajua Mimi waliosoma na wanaosoma pale wengi Wana vipato na tena Sio kutoka Pwani hao wa Pwanj Ht 1% hawafiki
Kuna St.Mary's Mazinde na Marian hizi Sio shule jamani km Sio za Kanisa ukipeleka mtoto ht km kafaulu intavyuu utaambiwa utoe pesa ya kushika nafasi ilikua 500k sijuii imeongezeka hyo apart from ada ya shule


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kampuni mara nyingi hazitoi misaada kwenye hamna, vigumu kuwaona shule yenye majengo mabovu na sare zimechafuka na kuchanika, vyoo havitoshi. Positive effect itakayotokea hapo ni ndogo kibiashara kuliko wakienda shule inayojulikana. Kwanza mazingira mazuri yanaendana na hadhi ya kampuni, taarifa itafikika zaidi kama hapa kila mmoja anaijua Marian, pia matokeo chanya yataonekana kwa wazazi, watoto na watumishi. Mjue kuna shule hakuna mwanafunzi hata mmoja mwenye kadi ya benki yoyote.

Kingine ni dini, waumini wa dini zote hupenda kwenda kwa mkumbo na upendeleo kwa taasisi zinazowaunga mkono ndio maana Abdulmajid kahudhuria kwa Wakristo na kuchangia. Image inayotokea hapo ni kubwa kwa benki, mwaka mwingine wataenda shule ya Kiislamu au walishaenda, mwingine ya Lutheran.

Makampuni hayatoi misaada kwamba yanawapenda sana Watanzania. Corporate Social Responsibility ni strategic hutoi hela bila calculations. Hata wanasiasa hutomuona mbunge anahudhuria mahafali shule ya kata madirisha hayana vioo, mpaka iwe shule nzuri nzuri. Last year NMB walitoa msaada CCBRT wakati wangeenda hospitali za ndani ndani uko ambako madawa tu ni tatizo
Mamilioni ya ada za Marian yanapitia CRDB, so ni win-win situation
 
Fr. Bayo anaaminika sana hapa Kerege kwa mchango wake mkubwa wa kuwainua vijana wa hapa. Kwa maendeleo hajambo. Parokia ya Kerege na shule ya sekondari wavulana ni juhudi zake. Big up Bayo.
 
Back
Top Bottom