KERO NSSF boresheni eneo lenu la Kiluvya, lina vichaka, linatumika kama njia kwa Wanafunzi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest

​
Kuna eneo ambalo ni kama pori linalomilikiwa na Mfuko wa NSSF lipo huku Kiluvya kutokea kwa Sumaye mpaka Shule ya Secondary Makurunge, Wanafunzi wanapita mpaka mida ya usiku wakitoka shule na sio salama kwao.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Ukiangalia kwenye ramani kuna Barabara kubwa tu iliyo chini ya TANROADS na ni kipande kifupi tu, kwa nini wasikitengeneze kipande hicho watoto wetu wakawa salama?

Ukiangalia vizuri kwenye picha utaona alama ya mwanzo na mwisho wa barabara inapotakiwa kuchongwa🙏

Barabara ikichongwa itasaidia usalama hata Bajaji zitakuwepo kutokea Madukani mpaka Shuleni, eneo la NSSF hawawezi kuweka uzio kwa kuwa maeneo yao mengi huwa wanakuja kuyakata viwanja na kuuza baadaye, au kama watayauza haya maeneo kwa sasa ni sawa tu maana ardhi yake ishapanda thamani huku wanaweka tu pori.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…