Uchaguzi 2020 NSSF: Hii siasa hapa kwenye daraja la Kigamboni ni sawa?

Uchaguzi 2020 NSSF: Hii siasa hapa kwenye daraja la Kigamboni ni sawa?

willpower

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2019
Posts
408
Reaction score
2,314
Jumatatu niliamua nipite daraja la Kigamboni kuelekea mjini. Nilipofika pale sehemu ya kulipia (Toll Centre) nikaona kuna picha za wanasiasa wawili zimebandikwa kwenye nguzo.

Hizi ni picha za ndugu John Joseph Pombe Magufuli (kwa wasiofahamu huyu ni Mgombea urais kupitia CCM) na ndugu Faustine Ndugulile (mgombea ubunge kupitia CCM).

Nafahamu ile ni ofisi ya umma, je kubandika picha za Wagombea ni sawa?

Je, wakija CUF ama ACT Wazalendo na picha zao nao pia watabandika bila kikwazo chochote?

Naamini uongozi wa NSSF hapo Kigamboni darajani mtanipatia majibu ambayo yanaweza kusaidia vyama vingine pia kuja kubandika picha za wagombea wao kwenye hilo eneo la kulipia.
 
Taasisi nyingi za umma zinatumika vibaya sana na hawa CCM.

Kwa mfano Tanesco imeruhusu nguzo zao za umeme zitumike kufunga kamba cross the road ili bendera za CCM zipepee...angekuwa CDM ama ACT nafikiri ni kesi ya kuhujumu miundombinu.
 
Mimi jana mchana nikiwa kwenye foleni pale Fire mbele yangu upande wa Barabara ya Mwendokasi niliona Gari Toyota Prado rangi ya Nyeusi kwenye plate number zake mbele na nyuma zikiwa zimezibwa kabisa na karatasi za kubandika zilizoandikwa T JPM 2020. Nikajiuliza je Sheria inaruhusu kufanya hayo?
 
Taasisi nyingi za umma zinatumika vibaya sana na hawa CCM.

Kwa mfano Tanesco imeruhusu nguzo zao za umeme zitumike kufunga kamba cross the road ili bendera za CCM zipepee...angekuwa CDM ama ACT nafikiri ni kesi ya kuhujumu miundombinu.
Huu ndiyo ukweli
 
Mabango ni ya kampuni binafsi na yako kibao kila eneo kawalipe na wewe wakuweke
Angalia chini ya bango utaona jina la kampuni
 
Mabango ni ya kampuni binafsi na yako kibao kila eneo kawalipe na wewe wakuweke
Angalia chini ya bango utaona jina la kampuni
Hata nguzo pia?? Muewe mleta mada. Kuna saa mnashindwa kujustify mambo kama haya mnabakia kutoka nje y mada. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hata nguzo pia?? Muewe mleta mada. Kuna saa mnashindwa kujustify mambo kama haya mnabakia kutoka nje y mada. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ndizo zipi za umeme za Tanesco ambazo kila mtu hubandika au zip?
 
Back
Top Bottom