Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linaonekana kuwa hoi kifedha, kwa miezi kadhaa sasa limekuwa likishindwa kuwalipa wastaafu malipo ya pensheni kwa wakati ambapo malipo hayo hufanyika tarehe 24.
Mwanzo ucheleweshaji huo shirika lilikuwa likidai kuwa unafanywa na shirika la Posta hata hivyo hakuna hatua zilizowahi kuchukuliwa.
Kutokuwepo uhakika wa tarehe ya malipo kumewafanya wastaafu washinde kwenye ofisi za Posta kwa kati ya siku mbili mpaka sita! Mimi nikiwa mmoja wa wahanga ambao tungelipwa tarehe 24 mpaka leo tarehe 28 malipo yameshindikana na hakuna taarifa yoyote kuhusu hali hii.
Kinachoonekana ni kuwa malipo yatafanyika baada makusanyo ya michango toka kwenye makampuni.
Ni vizuri shirika lijitokeze na kuwaeleza wateja kuhusu kadhia hii badala ya kujificha na kuwaacha wastaafu wakihangaika.