Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu futa hii kauli ya kubadilisha mara kwa mara uongozi ni shiiiida, nadhani nimeeleweka
Sent using Jamii Forums mobile app
We si tajiri mchangie sasa acha maneno ya kwenye kangaMzee kwanza shikamoo , halafu pole sana kwa yaliyokukuta , hii nchi kwa sasa inaenda kama gari lililokatika senta bolti , vumilia tu mzee wangu Mungu atakuokoa
Miaka 7 bado yupo madarakani Mungu atusaidie tu miujiza itokee kea kweli .Tushukuru kwankila Jambo enzi za JK tulilalamika wee mpaka Basi Sasa tumepata size yetu
Hii ndiyo sababu ya kuyaunganisha mashirika haya kwa nguvu za kisheria ili kuficha ukweli huu. Si NSSF tu PSPF nayo ilikuwa/ipo ICU.Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linaonekana kuwa hoi kifedha, kwa miezi kadhaa sasa limekuwa likishindwa kuwalipa wastaafu malipo ya pensheni kwa wakati ambapo malipo hayo hufanyika tarehe 24.
Mwanzo ucheleweshaji huo shirika lilikuwa likidai kuwa unafanywa na shirika la Posta hata hivyo hakuna hatua zilizowahi kuchukuliwa.
Kutokuwepo uhakika wa tarehe ya malipo kumewafanya wastaafu washinde kwenye ofisi za Posta kwa kati ya siku mbili mpaka sita! Mimi nikiwa mmoja wa wahanga ambao tungelipwa tarehe 24 mpaka leo tarehe 28 malipo yameshindikana na hakuna taarifa yoyote kuhusu hali hii.
Kinachoonekana ni kuwa malipo yatafanyika baada makusanyo ya michango toka kwenye makampuni.
Ni vizuri shirika lijitokeze na kuwaeleza wateja kuhusu kadhia hii badala ya kujificha na kuwaacha wastaafu wakihangaika.
Wazee hawa ndio wanaosema vijana wakalime na vijana wana tamaa. Ngoja dawa iwaingie Kwanzaa ili na sisi vijana wa sasa ivi tujue cha kufanya kwa family zetu zijazo na sisi kwa ujumlaIla siku hizi yataka moyo kuwahurumia the aged/wazee, maana ndio washabiki wakubwa wa ccm
Wewe unapingana na tafiti? TWAWEZA walisemaje?Ni kauli ya kibaguzi..ni kauli yenye mwelekeo wa itikadi ya ufashisti...Inaelekea hujafanya utafiti.CCM ina vijana wengi mashabiki...CCM ina wanawake wengi mashabiki..CCM ina mashabiki kutoka makundi yote ya jamii...Kauli za aina hiyo kama yako ndio anbazo hukosesha kura upinzani..Kauli nyingine ambazo hukosesha kura kwa upinzani ni kama zile za kusema mikoa ya Dodoma, Singida na kadhalika haijitambui na ikonyuma kimaendeleo na ndiyo maana inaipigia kura CCM na kwamba eti mikoa inayoitwa ya 'kaskazini' ina watu wanaojitambua na ndiyo maana inawapakura wapinzani....wapinzani lazima mjifunze....muwe na lugha nzuri na staha...
Serikali inapokopa toka mifuko ya jamii inatumia kigezo gani? Yaliyotokea NPF ya watu binafsi kukopa yanaweza kutokea sasa. Mbona wenyefedha zao hawakopeshwi? Mwisho kwanini NSSF hawakutani na wastaafu ambao tumekuwa tukienda kwenye ofisi zao na kupewa majibu ya dharau?Ni kwa sababu za kiutawala tu maana ndani ya miaka miwili mabadiliko mara mbili, sasa kila anaekuja lazma ajiridhishe na malipo yanayofanywa,hata rais JPM alipoingia madarakani alianza kuhakiki uhalali wa madai ya makandarasi,wengine hadi sasa hawajalipwa.Kubadilisha mara kwa mara uongozi ni shiiiiiiiiiiiida
kwani yeye ndio alijenga migorofa isiyo na wapangaji?
Ni kweli, ila ajabu hata sisi wanachama wanatutreat kama mijusi yaani mwaka sasa nadai michango yangu na sijaambulia kitu. WanalaanaNSSF haikuanzishwa kwa ajili ya kujenga viwanda, huu ni mfuko wa jamii na pesa zilizomo ni za wanachama si za serikali hivyo zinahitaji udhibiti wa kibenki. Kwa bahati mbaya zipo dalili zinazoleta mashaka juu ya mwenendo wake na hasa kutokuwepo wastaafu kwenye bodi yake pia kutokuwa na mawasiliano ya aina yoyote na wastaafu.
Hivi huwa si wanachukua pesa zetuShirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linaonekana kuwa hoi kifedha, kwa miezi kadhaa sasa limekuwa likishindwa kuwalipa wastaafu malipo ya pensheni kwa wakati ambapo malipo hayo hufanyika tarehe 24.
Mwanzo ucheleweshaji huo shirika lilikuwa likidai kuwa unafanywa na shirika la Posta hata hivyo hakuna hatua zilizowahi kuchukuliwa.
Kutokuwepo uhakika wa tarehe ya malipo kumewafanya wastaafu washinde kwenye ofisi za Posta kwa kati ya siku mbili mpaka sita! Mimi nikiwa mmoja wa wahanga ambao tungelipwa tarehe 24 mpaka leo tarehe 28 malipo yameshindikana na hakuna taarifa yoyote kuhusu hali hii.
Kinachoonekana ni kuwa malipo yatafanyika baada makusanyo ya michango toka kwenye makampuni.
Ni vizuri shirika lijitokeze na kuwaeleza wateja kuhusu kadhia hii badala ya kujificha na kuwaacha wastaafu wakihangaika.