Mwanzo ilikua ukimaliza mkataba wako secta binafsi unaruhusiwa kuchukua mafao yako yote. Lakini sasa upo utaratibu ambao nashindwa kujua kwa nini umeletwa. Mimi nilifanikiwa kuweka michango yangu kwa miaka kadhaa nssf wakati nafanya kazi secta binafsi. Baada ya kupata ajira ya serikali nilikua tayari nina salio la kama mil 10. Sasa nimetaka kuzichukua ili zinisaidie kwenye ujenzi ambao nimeuanzisha. Nimeenda nssf nikaambiwa kua hela yangu siruhusiwi kuichukua na kwamba itaunganishwa kwenye mafao ya mfuko wa serikali psssf pindi nitakapostaafu. Mimi binafsi naona hii si sawa maana mkataba wa kazi ulishaisha. Wadau wa jamii forum mnalionaje hili