NSSF, mbona Mafao yenu kiduchu kuliko wenzenu?

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Nimekuwa nafuatilia hii mifuko, ki ukweli naona mfuko ulio ekeza miradi kuliko yote ni NSSF ila naona ndio mfuko wenye Mafao ya mwisho kidogo kuliko mingine.

Naomba mwongozo kwa anayefahamika Remark; lkumbukwe kuwa hapo zamani wafanya kazi wote wa sector binafsi walitakiwa kujiunga NSSF ni hivi karibuni tu wafanya kazi wameruhusiwa kujiunga kwenye mifuko wanayoipenda.
 

Pia na hayo mafao mpaka uyapate, jasho itakutoka.
Kwanza lazima 'usubiri' ipite miezi sita baada ya kuacha kazi.
Halafu ukianza kudai mafao yako, hapo ndio utajuta kuwafahamu NSSF...
 

Iko hivi,

Kama ulivyosema hapo kabla, hawa NSSF ndio waliokua na jukumu la kuhusika na wafanyakazi wa sector binafsi ambao ki-idadi ni wengi sana kuliko Kada zingine!

Sasa basi kwakua Kada hii ya sekta binafsi ina wafanyakazi wengi basi hata mapato yake kutokana na monthly contributions yalikua ni mengi sana. Na kwakua Sheria hairuhusu mfanyakazi au mwanachama kuhama mfuko basi ni wazi kua faida ile ya shirika hili kua na wanachama wengi bado iko Mpaka leo.

Pia shirika hili linaendelea kuufaidi huo utaratibu indirectly hata kama ushafutwa sababu waajiri wengi wa hii sekta bibafsi wanaona uvivu kuanza kujihusisha na mifuko mingine ambayo awali haikuwepo, hivyo kila new staff wao wanamshauri aendelee kua NSSF, pia Rushwa from nssf to HRs inahusika nayo.

Kwa hiyo shirika linajikuta hata kama wasipotoa products nzuri, bado kwao linafanya vizuri in term of collections kwani lilishajikusanyia wanachama wa kutosha tu hapo awali wakati wa ukiritimba wa kuhodhi private sector.

Hawahitaji kujitangaza Wala kukuvutia sana sababu hata bila ya wewe tayari wao wanao wanachama wa kutosha tu ambao hawawezi kuwahama, na bado wanaendelea kupata wanachama wapya kupitia HRs ambao wameunga nao urafiki (Rushwa??!!)
 
Katika kipindi cha miaka kadhaa NSSF wamechezea sana pesa za walala hoi na uwekezaji usiokuwa na tija yoyote kwa wanachama bali wanasiasa wachache na mitandao ya ufisadi.
Nakuwa na wasiwasi kama wataweza kuweka mafaili wazi kwa ajili ya uongozi mpya hapo mbeleni!
 
Tunalipa wafanyakazi hela za kutosha kupitia michango yenu
 
Huwa nawashangaa waajiriwa wapya wanaojiunga na NSSF

Ni kutokujua mapema mkuu, sie tulioingia zamani sasa hivi tunajuta baada ya kufunguliwa masikio, na mbaya ndio hivyo huwezi kutoka.
 
Mm nilifanyaga field hapo waajiriwa wapya wanaletewa form za kujiunga bila kujua maana nssf huwa wanawahonga ma hr,, ila kweli nssf ni msikiti usiojulikana kwa wachache
 
We mdini kila jukwaa upo tu, Na ukiingia ofisi za TRA vipi.

Umejuaje kama kila jukwaa nipo km sio umbea...wadini wanaogeuza taasisi za umma kuwa taasisi zao za kidini kwa kuwabagua wengine....narudia tena ukiingia NSSF ni km umeingia kwny ofisi za BAKWATA!
 
Asanteni kwa kutufungua maskio kumbe LAPF ndio habari ya mujini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…