NSSF mmetupiga kitu kizito hapa Watanzania

NSSF mmetupiga kitu kizito hapa Watanzania

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Masha Mshomba Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), amebainisha mbele ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, changamoto kubwa iliyopelekea kuchelewa kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa hoteli ya kitalii ya nyota tano iliyopo jijini Mwanza eneo la Capripoint inayomilikiwa na NSSF ni kutokuwepo kwa muendeshaji hoteli wa kimataifa.​
1721641531403.png

Mshomba amesema hayo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyetembelea mradi huo tarehe 14 Juni, 2023. Hata hivyo amebainisha kuwa kuanzia mwezi Juni mwaka 2024 hoteli hiyo inatarajiwa kukamilika na kuanza kazi rasmi. Alisema katika uzoefu walioupata kwa wenzao wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya nchi Jirani ikiwemo Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe ni kwamba huwezi kumalizia hoteli ya nyota tano kabla hujapata muendeshaji wa hoteli.

Kwa mujibu ya Mshomba anadai kuwa bado hawajapata muendeshaji wa hoteli kipindi kile ndio maana mradi ulishindikana kukamilika, sasa kweli unaanzisha mradi ukiwa haujui nani ataendesha mradi tena kwa pesa za umma, sio pesa za Samia, sio pesa za Mpango wala sio pesa ya NSSF ni pesa za wananchi.

1721641565318.png


Alisema ilipofika mwaka 2017/18, Mfuko ulitangaza zabuni ya muendesha hoteli hata hivyo hakupatikana kutokana na mazingira ya kipindi hicho na mwaka 2019 mwezi Septemba walienda nchini Zambia na Afrika Kusini ili kupata uzoefu jinsi Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya nchi hizo inavyopata waendeshaji wa hoteli ambapo NSSF ilipata kampuni ya Hilton Hotels Worldwide, Radissons Hotels chini ya Radisson Hospitality, Inc na Legacy Hotel walio chini ya uongozi wa kampuni ya Antique Legacy Hotel, ila bado mpango wao ukafeli.

Hawataki kusema ukweli ila kuendesha hoteli za kimataifa ndani ya Tanzania ni mzigo mkubwa ambao kampuni za kimataifa zimeona hakuna faida, mizigo ya kodi na ushuru tena isiyo na kichwa wala miguu na ukosefu wa mipango ya muda mrefu ya kupata wateja haswa maeneo ya Kanda ya Ziwa. Unamleta Mzungu kutoka Uholanzi kuja Ilemela kutazama Mamba na Kenge kwenye Hifadhi ya Saanane, je kuna vitu vingine vya ziada vya kumfanya arudi tena Mwanza?
1721641592927.png


Hilton Hotels Worldwide ina jumla ya hoteli zaidi ya 24 ambazo zina matawi yake kwenye maeneo zaidi ya 7,600 kuanzia Marekani, Uchina, Afrika ya Kusini na kadhalika, kiufupi ni sehemu za kimkakati zenye kurudisha faida kwao. Huyu HHW hawezi kuweka nguvu zake kwenye eneo ambalo halina faida kwake (elewa neno faida).

1721641636063.png


Jumatatu, Mei 20, 2024 RC Mwanza. Mheshimiwa Said Mtanda alihimiza kukamilishwa kwa ujenzi hoteli ya nyota tano huku kukiwa hakuna mikakati yoyote ya msingi ya kulifanya hilo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya jiji la Mwanza upo ofisini kwako, je hili haulioni au ni maagizo kutoka juu kuwa ukae kimya?

Mwanzoni kabsa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Patrobas Paschal Katambi alitoa maelezo kuhusu taratibu za kupitisha miradi mbalimbali ambayo hupitia Benki kuu ya Tanzania (BOT) ili ishauri na ofisi ya Waziri Mkuu inasimamia na kuwa lengo kuu la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni kuwekeza kulinda fedha za mifuko, sasa mpaka sasa hivi hakuna chochote kinachoendelea na pesa za umma zimetumika.​
1721641702755.png

Meneja Usimamizi wa Miradi NSSF, Mhandisi Helmes Pantaleo unatoa maelezo ili kulinda ugali wako au kuonesha ukweli watanzania kuwa mradi wenu ni ghost project? Tanzania ndo mahala pekee ambapo mradi ukapigwa nakshi nje ili Rais na wateule wake wapate kufurahia na kuouga picha ili tu walipwe posho na kazi iendelee. Hoteli ya kitalii ya nyota tano yenye ghorofa 16, vyumba 168 vya kulala ila mpaka sasa hakuna cha msingi kinachoendelea.

Kwa Mwanza hapo mmetupiga kitu kizito, hoteli za Gold Crest, Mwanza Hoteli, Isamilo Grand Hotel zitaendelea kupata wateja na kupata manufaa kwa kuwa zinaendeshwa na watu binafsi, sasa hii hoteli ya kimataifa ya NSSF ndo mradi upi au ndo nyuma yake watu wanapiga pesa tu? NSSF hamna uwezo wa kuendesha hoteli ya kitalii wala kitu mfano wa hicho. Ninyi pamoja na TRA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji ikae chini na kuunda kamati maalamu ambayo itaweka mazingira bora kuruhusu waendeshaji wakubwa wa sekta ya ukarimu na hoteli kuja kuwekeza.

1721641793930.png


Sekta ya kisasa ya hoteli kwa dunia ya sasa ni zaidi ya kutoa tu malazi na chakula kizuri na kitamu. Unahitaji kutoa uzoefu wa kiubunifu wa moja kwa moja kwa wageni wako kwa kutambua mahitaji na matarajio yao kabla na baada ya ujio wao. Tengeneza mahusiano bora baina ya mahoteli na miundombinu ya eneo husika. Mfano, Mwanza tu, hakuna sehemu ya maegesho ambayo haina wafanyakazi wa TARURA wakiwa tayari kuchukua ushuru, yaani ukiegesha tu ugari dakika kadhaa unakutana na kadada kameshaandika mkeka wake.

1721641895236.png


Mwanza nzima hakuna sehemu maalumu za watu wenye mahitaji yao, hakunavyoo vya umma, hakuna free smoking areas (maeneo huru ya kuvuta sigara na bidhaa za tumbaku). Na kitu cha msingi zaidi ni kuiboresha miundombinu ya Uwanja wa ndege wa Mwanza, ili uweze kuruhusu ndege kubwa kutua moja kwa moja, hakuna ulazima wa mtu kufika Julius Nyerere International Airport halafu atafute tena usafiri wa kuja Mwanza, hapo ni zaidi ya kilomita 1,137, na sio kila mgeni anaweza kuunganisha moja kwa moja mpaka Mwanza kwa ndege kwa Precision Air.

1721641974327.png


Katika makutano ya barabara zetu kuna nafasi kubwa ya kutangaza vivutio vyetu kwa wasafiri, Makutano ya Nyerere, Kisesa- Igoma, wekeni billboards za kutosha. Tengenezeni bajeti ya kupanua uwanja wa ndege wa Mwanza, kuna eneo kubwa sana ukiwa unaelekea Igombe, na linatosha kuweka terminal ambazo zinaweza kuruhusu wageni wengi kuja kutembelea sehemu zingine za Tanzania ukiachilia mbali Dar es Salaam na Arusha. Hatma ya maendeleo ya uchumi wa Tanzania yapo mikononi mwetu.
SIO KWA UBAYA! ILA NSSF MMEKULA PESA HAPA!
 
Lakini kuna investment nyingi Mkuu sio real estate tu! Hata transportation pia ni investment nzuri
Nimesema hivi mifuko yote ya pension ata WCF( workers compensation fund) wao wanafikili uwekezaji ni real estate, fixed deposit na governent bond wakati kuna uwanja maana wa uwekezaji wenye faida ili kuweza kulinda pesa za wanachamawake. Kuna majengo mengi wamejenga lakini hayana wala gani na kila mwaka wanayatengea bajeti ya maintainace and repair.
 
Nimesema hivi mifuko yote ya pension ata WCF( workers compensation fund) wao wanafikili uwekezaji ni real estate, fixed deposit na governent bond wakati kuna uwanja maana wa uwekezaji wenye faida ili kuweza kulinda pesa za wanachamawake. Kuna majengo mengi wamejenga lakini hayana wala gani na kila mwaka wanayatengea bajeti ya maintainace and repair.
Ndio Mkuu hapo nimekuelewa
 
Omary Mziya sijui alikuwa wapi mzee wangu?! Yaani Director of Operations halafu anaruhusu huu upupu uwatoe upele wananchi?! Ibrahim Maftah alishindwa kabsa kunusa hatari ya hasara?
 
Huu mradi ni 🐘 Nimeona sasa hivi wanajenga ngazi za nje, yani mpaka hoteli inapakwa rangi hawakujua kutakuwa na uhitaji wa External Stairs.
Wiki iliyoisha nilipita hapo nikiwa na vijana wangu yaani tulikuwa tunacheka kama mazuri vile. Nilivyoaambia kuwa ni pesa za Umma nikaona wamebadilika.
 
Aibu ya Mwaka!

Anayeamua matumizi investiments mifuko hii nani? Na akikosea anachukuliwa hatua gani? Na wangapi waliokosea wakachukuliwa hatua na ni miaka gani?
Ukweli ni kwamba mwanza hina uhitaji wa Hoteli kubwa namna hii! Tumekurupuka!
 
Aibu ya Mwaka!

Anayeamua matumizi investiments mifuko hii nani? Na akikosea anachukuliwa hatua gani? Na wangapi waliokosea wakachukuliwa hatua na ni miaka gani?
Ukweli ni kwamba mwanza hina uhitaji wa Hoteli kubwa namna hii! Tumekurupuka!
 
Back
Top Bottom