NSSF na habari njema...

NSSF na habari njema...

TAMU YA LEO

Member
Joined
Mar 26, 2020
Posts
8
Reaction score
3
Moshi

Vikundi vya wajasiriamali wadogo wadogo mkoani Kilimanjaro vipo mbioni kunufaika na mkopo wenye riba nafuu uliotolewa na serikali kupitia shirika la hifadhi ya jamii Nssf kwa lengo la kuinua biashara zao.

Shirika hilo limetenga shilingi bilioni tano kwa ajili ya kuvikopesha vikundi hivyo ambapo walengwa wakuu watakuwa ni wanawake pamoja na vijana ambao wapo kwenye vikundi vilivyosajiliwa kwa mujibu wa sheria.

Meneja wa NSSF mkoa wa Kilimanjaro Large Materu alisema hadi sasa zoezi linaloendelea ni kuorodhesha vikundi hivyo vilivyopo katika wilaya zote na kuvifanyia upembuzi yakinifu.

''Tunaendelea kuviorodhesha hivi vikundi toka katika halmashauri zote baada ya hapo tutaangalia vile ambavyo vimekidhi vigezo tuweze kuwapa huo mkopo''alisema.

Kwa mujibu wa meneja huyo ni kuwa wanufaika wa mkopo huo ambao utakuwa wa gharama nafuu ni lazima wajishughulishe na shughuli ndogondogo za uzalishaji mali lengo likiwa ni kuwainua kiuchumi.

Alisema shirika la viwanda vidogo vidogo (SIDO)na chuo cha ufundi stadi (VETA)ndio waliopewa jukumu la kusimamia aina ya uzalishaji unaofanywa na kikundi kabla ya kuidhinishiwa mkopo huo.

''Vigezo vya kupata huu mkopo ni rahisi sana angalau wanakikundi wawili wawe ni wanachama hai wa nssf na kama inavyofahamika kiwango cha chini cha uchangiaji ni elfu 20"alisema.

Mwenyekiti wa kikundi cha Malengo Josia Kyara alisema mpango huo wa serikali ni mzuri kwani utawezesha kukua kwa wajasiriamali wadogo ambao wengi walisumbuliwa na shida ya mtaji.

''Hii ni fursa mpya kwetu sisi wajasiriamali ambapo wengi tulishindwa kusonga mbele kwa kukosa mitaji ni dhahiri tutaenda kupiga hatua kubwa katika uzalishaji kwa siku chache zijazo''alisema.

Mwisho.
 
Kwani hili shirika lishamaliza kulipa wateja wake au ndo linakupoesha ili lipate taji wa kulipa.
 
giphy.gif
 
Kwanini Kilimanjaro?? Is this political??
Kwanini siyo Songea, Kilwa, Ifakara, Ngara....Au hili shirika huko halina matawi??

Waache mbwembwe walipe wastaafu!

Everyday is Saturday......................... 😎
 
Back
Top Bottom