NSSF wabadili sheria yao ya kutoa mafao

NSSF wabadili sheria yao ya kutoa mafao

Pawepo na mashirika mengine yenye ushindani
Huko sio kwenye biashara ya makampuni ya simu!!na mchawi ni serikali tu,kukomba pesa zote huko kwa matumizi yake,na kutu kingine ni pesa ya wastafu kutumika kwenye vitega uchumi vyenye hasara tu
 
Kwanini mtu anayeacha kazi kwa hiari na alikuwa mwanachama halali wa Nssf hawezi kupewa hela zake mpaka afikishe miaka 55 Yaan umri wa kustaafu?

Mbona kama hii sheria inafavor zaidi upande wa NSSF na sio mwanachama. Kwanini mtu anayefukuzwa au kuachishwa kazi na muajiri ndiyo anapaswa kupewa?

Kwahiyo tuseme kuwa mtu hana haki ya kuacha kazi na akastahili kupewa fedha yake akaendelea na maisha mengine?

Inakuwaje hela mlizokata kwneye mshahara wangu mnipangie namna ya kuzichukua? Kwann nisichukue wakati wowote?
Huu ni utapeli na unyanyasaji kwa watumishi
 
Watukutu siku zote hupata tabu kutokana na tabia zao,kwanini ufukuzwe?
kwa nini uache kazi kama sio umeiba au una kazi nyengine.
 
Hii sheria wakati inajadiliwa bungeni Mhe Easter Bulaya na wengine wachache walipambana vikali kuipinga lakini bahati mbaya wafanyakazi huku mitaani wakawa hawana time, wako bize kumsifia jiwe wakati huo. Kuja kushtuka tayari keusi kekundu watu wanakumbuka shuka kumekucha... hatutaki kabisa kufuatilia miswaada yenye athari kama hii ikiletwa bungeni.
Tatizo Ester ni covid 19
 
Ukisoma kichwa Cha Mada, unaweza kudhani tayari Kuna mabadiliko.
Kweli uandishi kazi.
Iko hivi, hii sheria ilibadilishwa tokea kipindi cha jiwe,ndipo walipofuta rasmi fao la kujitoa kwa mifuko ya hifadhi za jamii. Badala yake wakaweka utaratibu kwamba kama umeachishwa kazi na ikapita miezi 6 huna ajira unaenda kuomba kulipwa sehemu tu ya mafao yako kwa kipindi fulani tuu basi. Watu walilalamikia sana hii kitu pamoja na kile kikokotoo...
 
Back
Top Bottom