NSSF yajivunia trilioni 7.3 ukusanyaji wa michango ya wanachama kwa mwaka wa fedha 2022/2023

NSSF yajivunia trilioni 7.3 ukusanyaji wa michango ya wanachama kwa mwaka wa fedha 2022/2023

Joined
Apr 9, 2022
Posts
66
Reaction score
32
Phoenix20220822_125227.png

Kiasi cha shilingi Trilioni 7.3, katika mwaka wa fedha 2022/2023, kimekusanywa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambapo fedha hiyo inatokana na michango ya wanachama wa mfuko huo.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw.Masha Mshomba wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya NSSF kwa Mwaka wa fedha 2021/ 2022.

Hata hivyo Mwaka wa fedha ulioishia mwezi Juni 2022, NSSF imefanikiwa kukusanya shilingi trioni 6.2. kiasi ambacho kimeimarisha maradufu utoaji wa huduma kwa wanachama.

Bw.Mshombe amesema kwamba kwa Mwaka huu wa fedha 2022/2023 NSSF imejiwekea vipaumbele kabambe ili kuufanya Mfuko huo kuendelea kuimarika zaidi ikiwemo kuongeza wanachama kutoka sekta rasmi na isiyo rasmi, kuboresha njia za kukusanya na kuwasilisha michango kwa njia yakieletroniki(TEHAMA),kuboresha huduma kwa wanachama,kufanya uwekezaji salama nakuepuka upotevu wa fedha ili kuweza kulipa mafao kwa wanachama.

"NSSF inaendelea na ukamilishaji wa miradi yake ikiwemo kukamilisha ujenzi wa jengo la biashara lililopo mkoani Mwanza,pamoja na jengo lililopo Mtaa wa Mzizima,Mradi wa Nyumba za Kupangisha na kuuza huko eneo la Dungu, Kigamboni,Tuangoma na Kijichi Wilayani Temeke ,pamoja na kiwanda cha Sukari kinachojengwa Mkoani Morogoro ambacho kinatarajiwa kukamilika mwaka wa fedha 2022/2023" alisema Mshombe.

Aidha pamoja na mambo mengine Mkurugenzi Mkuu huyo wa NSSF amesema Kwamba wanaendelea na uimarishaji wa usimamizi wa Mapato ili kuahakikisha fedha hizo zinatumika kwa matumizi stahiki ili kuleta ustahimilivu wa mfuko,ambapo mfuko huo unatakiwa kutumia asilimia 10 pekee ya mapato yanayokusanywa na mfuko huo
 
Back
Top Bottom