Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema hadi Oktoba 31, mwaka huu utakuwa umekamilisha hatua zote za uuzaji wa Mradi wa Dege Eco Village kwa karibu Dola 220 milioni za Marekani (zaidi ya Sh501 bilioni). Mradi huo uliopo Kigamboni, Dar unapata mteja ikiwa ni baada ya ujenzi wake kusimama kwa zaidi ya miaka saba tangu Januari 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mshomba leo Septemba 25, 2023 amesema Mradi huo umeuzwa kama ulivyo bila kumtaja mnunuzi kutokana na taratibu kubana, ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Bodi ya Mfuko na Serikali ili kurudisha fedha za wanachama zilizowekezwa awali katika mradi huo.
Kwa mujibu wake, hadi uamuzi wa kuuzwa mradi huo unafikiwa tayari ulikuwa umeshatumia zaidi ya Sh330 bilioni huku akieleza kuwa kwa mnunuzi waliyempata watakuwa wamepata faida.
Hatari thana... AIP01SBV0DQ Imethibitishwa.Umepokea Tsh50.00 kutoka 219777 - M-PESA FAIDA tarehe 25/9/23 saa 12:39 AM Salio lako ni M-Pesa ni Tsh70.30.
Kuna yule Azimio aliingia ubia na NSSF na kuithaminisha ardhi iliyotumika kwa bei ya kuruka mpaka akaingia kwenye ripoti za CAG, wamemalizanaje? Maana hisa zake zilikuwa 55%
Marehemu Abel Motika " Mr Ebbo" kwenye kibao chake cha maneno mbofu mbofu aliimba watoto wanafundishwa historia kuwa mzungu aitwaye Rebman ndio aligundua mlima Kilimanjaro na wakati kina Mangi walikuwepp hapo kila siku.
Kama watoto wanaanza kujazwa uongo kuhusu historia ya nchi wataachaje kudanganya mnununzi.
Igizo la royal tour tuliambiwa liligharimu bilion 7 eti zilichangwa na wadau ambao hawatajwi ila ukichunguza kiundani utajua kulikuwepo upigaji wa hali ya juu na hizo ni kodi za wananchi.