NSSF yauza Dege Eco Village Kigamboni kwa bilioni 501, mnunuzi afichwa

NSSF yauza Dege Eco Village Kigamboni kwa bilioni 501, mnunuzi afichwa

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema hadi Oktoba 31, mwaka huu utakuwa umekamilisha hatua zote za uuzaji wa Mradi wa Dege Eco Village kwa karibu Dola 220 milioni za Marekani (zaidi ya Sh501 bilioni). Mradi huo uliopo Kigamboni, Dar unapata mteja ikiwa ni baada ya ujenzi wake kusimama kwa zaidi ya miaka saba tangu Januari 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mshomba leo Septemba 25, 2023 amesema Mradi huo umeuzwa kama ulivyo bila kumtaja mnunuzi kutokana na taratibu kubana, ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Bodi ya Mfuko na Serikali ili kurudisha fedha za wanachama zilizowekezwa awali katika mradi huo.

Kwa mujibu wake, hadi uamuzi wa kuuzwa mradi huo unafikiwa tayari ulikuwa umeshatumia zaidi ya Sh330 bilioni huku akieleza kuwa kwa mnunuzi waliyempata watakuwa wamepata faida.
Kwa mujibu wake, hadi uamuzi wa kuuzwa mradi huo unafikiwa tayari ulikuwa umeshatumia zaidi ya Sh330 bilioni huku akieleza kuwa kwa mnunuzi waliyempata watakuwa wamepata faida.[emoji848][emoji2827]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Faida tupu wallah.. Jamaa wanakuja kufanya finishing tuu
7200f1_775e521490bb4392bdd7e89a235fe247.jpg
0f3c0dd55f6e1c40b5e8b17c04b587b7.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni jambo jema kama amepatikana mmiliki mpya. Sema tu hawana sababu ya kumficha huyo mnunuzi. Maana ni suala tu la muda kabla hajafahamika rasmi.
NSSF watapata ngapi
Dalali atapata ngapi
Chama ukizingatia kuna uchaguzi mkuu kitapata ngapi
Washika dau
Wazee watapata ngapi
Chawa watapata ngapi

Maokoto ni kuokoteza..! Kuna mifereji maji yake yanapita usiku tukiwa tumelala..(yazinkieyo nakio yaeemee kutekwa)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NSSF watapata ngapi
Dalali atapata ngapi
Chama ukizingatia kuna uchaguzi mkuu kitapata ngapi
Washika dau
Wazee watapata ngapi
Chawa watapata ngapi

Maokoto ni kuokoteza..! Kuna mifereji maji yake yanapita usiku tukiwa tumelala..(yazinkieyo nakio yaeemee kutekwa)

Sent using Jamii Forums mobile app
Kodi pia
 
Yani mnashangaa mnununzi kutotajwa?

Marehemu Abel Motika " Mr Ebbo" kwenye kibao chake cha maneno mbofu mbofu aliimba watoto wanafundishwa historia kuwa mzungu aitwaye Rebman ndio aligundua mlima Kilimanjaro na wakati kina Mangi walikuwepp hapo kila siku.

Kama watoto wanaanza kujazwa uongo kuhusu historia ya nchi wataachaje kudanganya mnununzi.

Igizo la royal tour tuliambiwa liligharimu bilion 7 eti zilichangwa na wadau ambao hawatajwi ila ukichunguza kiundani utajua kulikuwepo upigaji wa hali ya juu na hizo ni kodi za wananchi.
Royal tour, anuani za makazi vyote vimekufa watu wamepiga pesa wakakaa pembeni
 
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema hadi Oktoba 31, mwaka huu utakuwa umekamilisha hatua zote za uuzaji wa Mradi wa Dege Eco Village kwa karibu Dola 220 milioni za Marekani (zaidi ya Sh501 bilioni). Mradi huo uliopo Kigamboni, Dar unapata mteja ikiwa ni baada ya ujenzi wake kusimama kwa zaidi ya miaka saba tangu Januari 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mshomba leo Septemba 25, 2023 amesema Mradi huo umeuzwa kama ulivyo bila kumtaja mnunuzi kutokana na taratibu kubana, ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Bodi ya Mfuko na Serikali ili kurudisha fedha za wanachama zilizowekezwa awali katika mradi huo.

Kwa mujibu wake, hadi uamuzi wa kuuzwa mradi huo unafikiwa tayari ulikuwa umeshatumia zaidi ya Sh330 bilioni huku akieleza kuwa kwa mnunuzi waliyempata watakuwa wamepata faida.

Attachments

  • 704A2A67-752B-49F2-B20C-34D7B87C36D6.jpeg
    704A2A67-752B-49F2-B20C-34D7B87C36D6.jpeg
    31.4 KB · Views: 5
Back
Top Bottom