NSSF yauza Dege Eco Village Kigamboni kwa bilioni 501, mnunuzi afichwa

NSSF yauza Dege Eco Village Kigamboni kwa bilioni 501, mnunuzi afichwa

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema hadi Oktoba 31, mwaka huu utakuwa umekamilisha hatua zote za uuzaji wa Mradi wa Dege Eco Village kwa karibu Dola 220 milioni za Marekani (zaidi ya Sh501 bilioni). Mradi huo uliopo Kigamboni, Dar unapata mteja ikiwa ni baada ya ujenzi wake kusimama kwa zaidi ya miaka saba tangu Januari 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mshomba leo Septemba 25, 2023 amesema Mradi huo umeuzwa kama ulivyo bila kumtaja mnunuzi kutokana na taratibu kubana, ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Bodi ya Mfuko na Serikali ili kurudisha fedha za wanachama zilizowekezwa awali katika mradi huo.

Kwa mujibu wake, hadi uamuzi wa kuuzwa mradi huo unafikiwa tayari ulikuwa umeshatumia zaidi ya Sh330 bilioni huku akieleza kuwa kwa mnunuzi waliyempata watakuwa wamepata faida.

Wangeutekeleza Kuanzia Magomeni hadi Ubungo mataa
 
Mradi ulikua mzuri sana, tatizo rushwa na ufisadi ukweli ni kwamba vitu vingi wame vi write-off kulinda hadhi ya wakubwa waliohusika ila kwa gharama zile za ujenzi nyumba ya million 50 inajengwa kwa million 200 kutokana na kuongeza cha juu kwenye kila kitu, bado hujaweka wazee wa consultancy.
 
....Mradi huo umeuzwa kama ulivyo bila kumtaja mnunuzi kutokana na taratibu kubana .......... transparency n accountability ni changamoto sanaa
 
Pesa ndogo sana hizo, kwa mradi mkubwa hivyo.

Ikitakiwa uuzwe kwa 1 billion US Dollars

Toka Maktaba

20 Sep 2017
Mradi mkubwa wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni Dar es Salaam uitwao Dege Eco Village ulioanzishwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii 'NSSF' na kusimama ujenzi wake mwaka 2016 unapigwa mnada. Kuliripotiwa kuwepo kwa ufisadi wa zaidi ya TSH bilioni 179 katika mradi huo na sasa anatafutwa Mwekezaji atakaeuchukua.

Habari kumbukizi mwaka 2017, mradi wa Dege Beach Eco Village wapigwa mnada

Yono Auction Mart madalali maarufu Tanzania watangaza mnada wa mradi mkubwa baada ya NSSF kuishiwa fedha na hivyo mradi kukwama kuendelea.

Dhima ya mnada huo ni kupata mwekezaji awe wa ndani au nje ya nchi ili kuwezesha mradi huo uweze kukamilika.

Mradi huo una thamani wa USD 350 milioni hivyo anatafutwa mwekezaji kutia kiasi hicho cha fedha ili ukamilishwe kupitia mnada huo.

Kukamilika kwa ujenzi wa daraja la Kigamboni kulitegemewa kutasaidia pia uchochezi wa kiuchumi ktk mradi huo na maeneo ya Kigamboni, Dar-es-Salaam lakini wapi .
 
Royal tour, anuani za makazi vyote vimekufa watu wamepiga pesa wakakaa pembeni
Kila siku nasema mfumo wa nchi unsababisha watu wajinga waongoze wenye akili.

Mtu kama Nepi kwa uwezo alioonyesha tangu ajibebee vibendera vya kutosha kidato cha 4 ni jina la baba yake ndio kasafiria kufika hapo .

Katiba pendekezwa ya Warioba ilikuwa na kipengele cha mawaziri wasitokane na wabunge kitu ambacho CCM na genge lao hawataki sababu uwaziri ni cheo cha kulipana fadhila kwa Tanzania.

Hebu angalia mawaziri failure kama Kipara na Nepi utapata kuona nchi inaelekea wapi.
 
Nyie endeleeni kuhoji mnunuzi kapatikanaje
Tena kwa jeuri ya hela ataipiga chini yote halafu aweke kiwanda
Huu mradi utakuwa una nyufa kibao kila jengo
Acha nitafute tenda ya demolitions tu
Aisee huu mradi ulijengwa kisasa sana ni zege tupu na hamna nyufa hata moja, yaani ukipita hapo kama ww n mzalendo unajiuliza hizi hela mbona wamezitupa hapa
 
Kuna yule Azimio aliingia ubia na NSSF na kuithaminisha ardhi iliyotumika kwa bei ya kuruka mpaka akaingia kwenye ripoti za CAG, wamemalizanaje? Maana hisa zake zilikuwa 55%
Mi nahisi karudishiwa mradi wake bwana Yule
Ukakasi unaanza hapo pa kutotaja mnunuzi
Ila yote Heri ,Bora waendelee kujenga mji uzidi kutanuka na mizimu iondoke kwenye Yale magofu
 
Mradi ulikua mzuri sana, tatizo rushwa na ufisadi ukweli ni kwamba vitu vingi wame vi write-off kulinda hadhi ya wakubwa waliohusika ila kwa gharama zile za ujenzi nyumba ya million 50 inajengwa kwa million 200 kutokana na kuongeza cha juu kwenye kila kitu, bado hujaweka wazee wa consultancy.
Sure, it was one of the best Real estate project to be established in TZ
Shida ni ufisadi wetu maana Nina mashaka kama wale Azimio builders ambao walikua wabia wa Nssf sijui kama waliweka hata Senti yao
Uwezekano mkubwa walichukua Hela za Nssf pekee kutekeleza ule mradi
Vinginevyo,ulikua mradi mzuri saana
 
Kwani sheria za nchi yetu zinasemaje raia wa nje kumiliki ardhi hapa nchini kwetu? Si haziruhusu. Hata wale diaspora wetu hawaruhusiwi. Labda ndiyo maana wamemficha huyo aliyeuziwa na kumilikishwa hiyo ardhi na ukubwa wa ardhi hiyo umefichwa.
 
Huu mradi ndio uliofanya wafanyakazi wasipewe pesa zao eti hadi miaka 60 waliotafuna hela za wafanyakazi wengine wakazawadiwa ubalozi ili wakazitafune vizur
Ila Nssf wanatesa Sana watu
Mara wajenge nyumba ambazo zipo overrated Kwa kuongeza gharama za ardhi na vifaa
Mara wajitie kujenga viwanda
Kote huko wanatumia pesa za wanachama mwishowe wanashindwa kuwalipa mafao yao, wanakimbilia kutunga sheria kandamizi
Inaumiza sana
 
Back
Top Bottom