NSSSF wanavyotuumiza wanachama

NSSSF wanavyotuumiza wanachama

Captain mopao

Senior Member
Joined
Feb 25, 2021
Posts
133
Reaction score
384
Habari ndugu jamaa na marafiki.

Nilikuwa mfanyakazi katika taasisi binafsi hapa mkoani nimefanya kwa muda wa miaka miwili, ingawa ndoto zangu zilikuwa ni kujiajiri ktk biashara kwa hiyo niliweka target ya kufanya kazi kwa muda ili nipate mtaji wa kuanzia business.

Mwez wa pili mwaka huu nikaona ni wakati sahihi wa kufanya kile nilichokuwa nime plan, kwa pesa niliyokuwa nimeikusanya nikajumlisha pesa zangu za NSSSF nikaona zitanitosha kabisa.

Moja kwa moja nikaenda NSSSF kufungua madai nikaambiwa yanipasa nilete barua kutoka kwa mwajiri wangu, nikawasilisha barua yangu hapo mapokezi akapokea dada mmoja akaisoma kisha akaniambia nenda kwenye notice body kasome vigezo vya kufungua madai kisha jipime kama unastahili.

Nikasogea mpaka kwenye ubao wa matangazo sheria zilioandikwa pale ilibidi nilie tu ndugu zangu, kwanza natakiwa kuwa niliachishwa kazi au kustaafu sio mimi kuacha kazi pia nitapewa asilimia thelathini ya mshahara, yaani sheria nyingine hata nimezisahau nikarudi kwa yule dada nikamwambia inakuaje akasema jipime we mwenyewe umekidhi vigezo.

Jasho likaanza kunitoka yaani plan zangu zote ni zero nikaondoka kinyonge.

Pesa yangu inanitoa jasho kutafuta halafu hawa ndugu wanazila kiulaini kbsa mliotunga hizi sheria.

Mkumbuke kuna jehanamu ndugu zangu
 
Mitano Tena na tena. Nchi hii wabongo hatujawahi kuwa na ushirikiano, mmoja akipatwa Tatizo mwingine anaona halimhusu. Siku na yeye yakimkuta na anaanza kulialia, na akijifanya tu kupambana kwasababu atakuwa yuko peke yake atadhibitiwa kikamilifu.

Anyway, kama ulikuwa hujui leo limekukuta ndio umejua.

Hiyo sheria ilishatungwa muda tu na imeshaumiza wengi tu na bado itawaumiza wengi ambao huwa wanashangaa kwanini kuna watu wanaiona serikali ya Magu ni shetani.

Kosa la kwanza ulilofanya ni KUANDIKA BARUA YA KUACHA KAZI.

Utakachopewa hapo NSSF ni asilimia 33.3 ya mshahara wako kwa miezi 6, then utafute KAZI nyingine uendeleze mfuko wako au usubiri miaka 55 ndio uchukue chako.

One Nation- Two systems. Nchi moja lakini sheria inatungwa kwaajili ya watu fulani tu wengine haiwahusu.

Sheria wanatungiwa masikini tu, hiyo sheria ya mafao wabunge, vigogo na wanasiasa haiwahusu.

Nimalize kwa kusema: KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI. USIWASIKILIZE MABEBERU, HAWATUTAKII MEMA KABISA. TUKO VIZURI🤣
 
Hii mifuko ilitakiwa iwe Ni hiari ya mtu kujiunga.

Ili la kulazimisha kila mwajiriwa ukamtunzie kiinua mgongo chake kwa lazima.

Ni uhuni na unyanganyi wa Mchana kweupe wa vipato vya wafanyakazi.

Tatizo ni kwamba Serikali iliyopaswa iliweke sawa suala hili, ndio mnufaika mkubwa wa Unyanganyi huu.
 
Hio ni sheria ya NSSF wadau mmeijadili, tena mmeijadili vizuri sana, sasa tujee kwenye sheria za;

1) Makato Ya Mshahara (Payee, Income Tax, Social Fund n.k).

2) Kodi katika bidhaa mtu wa chini akinunua (VAT, SGR, NYERERE DAM, TANROAD, BANDARI, MAZINGIRA n.k).

Ukipiga mahesabu vizuri ya makato katika mshahara mtu anaopata pamoja na makato ya kodi katika bidhaa, basi nusu ya mshahara inaenda serikalini.

Halafu wabunge mliowachagua ndio wanaenda kuzipigia makofi na kuziunga mkono hizi kodi bungeni kipindi zikipitishwa.
 
Nikifikaga kwenye suala la nssf ua nakufa ganzi pole pole yan leo hii let say una miaka 30 umeamua kuacha kaz hela yako uiijie ukiwa na 55 ya nn sasa wana uakika gan ntakuepo kwa k vant hiz? bado hyo hela haiongezek ndio nini sasa
 
hivi kile kikokotoo kipya kinaanza kutumika lini.MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII
1.Ni mifuko inatumika kupunguza salaries
2.Ni sehemu ya serikali ya awamu ya tano kuchota mahela ya wanufaika ili kwenda kufund project zilizoanzishwa kimisifa
3.ONGEZA
 
Tunapowaambia mabaya ya CCM mnatuona sisi mazuzu na hatuna nia njema na taifa hili.ubaya wa watanzania ushabiki na ujinga vimetawala hatuamui mambo kwa utashi bali ushabiki. Hiki kikombe tutakinywea wote kwa style tofauti tu hakuna namna.
 
Daah. Yaani nchi hii watu wote wanaguswa kwa style tofauti kila mmoja.
 
Ukiona vipi rudi kwa muajiri wako ongea nae ili akuandikie barua nyingine ili uweze kuomba FAO LA KUTOKUWA na ajira ambalo utapatiwa asilimia 33.3 ya mshahara wako. Pambana muda bado unao.
 
Hivi uwa inachukua muda gani toka u submit details zote enikichefuchefu mpaka pesa inatoka?

Pia wana hili la kutaka NIDA ID, na watu wana namba tu za NIDA, hili limekaa vipi kwa wajuzi!?
 
nkfkaga kwenye suala la nssf ua nakufa ganz pole pole yan leo hii let say una miaka 30 umeamua kuacha kaz hela yako uiijie ukiwa na 55 ya nn sasa wana uakika gan ntakuepo kwa k vant hiz? bado hyo hela haiongezek ndio nn sasa
Ile wanaiwekeza kwenye miradi ina maana inazalisha cha ajabu unakuja kupewa ela yako ile ile ulioiacha miaka kumi au ishirini nyuma. Wizi huu unaumiza sana wananchi wa chini.
 
shida hapa ni maccm maana matumbo yao yamekuwa makubwa halafu hatuoni hata wanachokifanya iweje mbunge asikatwe na yeye? kwanini tunafanyizana hivi? CCM Itakapotoka madarakani ndio haki zetu zitakapopatikanika wamekaa hawabuni miradi wao ni kuangalia wachukueje hela kwa wananchi.
 
Pole sana sasa nakushauri mfuate mbunge wako umpe haya malalamiko.
 
Jamani mwenye namba ya mwenezi pole pole katika kile kipindi chake channel ten usiku.. huwa anakuwa live. Ukiwa na shida unapiga inatatuliwa hapo hapo... Nomba mwenye nayo aiweke hapa ili jamaa pamoja na wengine wenye shida tuitumie kupeleka vilio vyetu kwake... Asante..
 
Ukiona vipi rudi kwa muajiri wako ongea nae ili akuandikie barua nyingine ili uweze kuomba FAO LA KUTOKUWA na ajira ambalo utapatiwa asilimia 33.3 ya mshahara wako. Pambana muda bado unao.
Hilo ni gumu, maana kufukuzwa kazi huwa kunaendana na fidia ya mshahara wa mwezi mmoja mbele bila kufanya kazi.

Ndio maana makampuni mengi huwa yana tabia ya kuku- frustrate wewe ndio uandike barua ya kuacha kazi ili yakwepe hasara.
 
NSSSF ndio nini? Alafu kwa ujinga wako umeirudia zaidi ya Mara mbili, kuonyesha kuwa kweli wewe hujui unachozungumza.
Ninakushauri hata hiyo biashara usiende kufanya
 
Mitano tena na sasa wanataka kumwongezea 7 .
 
Back
Top Bottom