Pre GE2025 Ntobi aomba radhi kwa kauli zake kuhusu Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Ntobi, ameomba radhi kufuatia kauli zake alizotoa kuhusu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu. Ntobi ameeleza kuwa kauli hiyo ilisababisha mjadala mkali usio na afya ndani ya chama.

"Ni wazi kwamba nilihamanika tu," alisema Ntobi. "Naomba radhi sana kwa Chama, wanachama, viongozi wa ngazi mbalimbali, Watanzania, na kwa bosi wangu, Tundu Lissu."

Soma, Pia: Alichoandika Mnyika: Maneno ya Ntobi si msimamo wa Kamati kuu Wala CHADEMA na mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti huyo yako chini ya Kanda

Ntobi amesisitiza kuwa anawajibika kwa makosa yake na ameonyesha masikitiko makubwa kwa kauli hiyo. “I’m deeply sorry,” alihitimisha.


Baadhi ya Tweets zenye kauli za Ntobi kuhusu Tundu Lissu akionyesha wazi hakubaliani na Lissu kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA


 

Nasikia ni professor wa siasa pia
 
Ntobu,MMM na Boni yai ni kikundi cha wahuni na wanufaika wa Maovu ya CCM kujifanya wanaharakati kumbe machawa na hawajui wanatetea nn....binafsi nilikuwa nawakunali ila sahivi wamekuwa takataka.
Ntombi (siyo Ntobi), Yericko Nyenyere (siyo Nyerere), Bonge (siyo Boni) Yai (mwili mkubwa akili kisoda), hawa ni machawa wa Mbowe ambao akili inawaza matumbo yao
 
Ntobu,MMM na Boni yai ni kikundi cha wahuni na wanufaika wa Maovu ya CCM kujifanya wanaharakati kumbe machawa na hawajui wanatetea nn....binafsi nilikuwa nawakunali ila sahivi wamekuwa takataka.
Nyie si mliamini mayai yanaweza jenga ghorofa?
 
Lakini si ni ukweli alipigwa kwenye kura za maoni na Nyalandu? Si mnasema Lisu anaongea ukweli naked na huu hapa ni naked kubalini tuu 😆😆
 
Alichokiandika awali ndio msimamo wake, haya mengine ni kujikosha tu.
 
hahahaaaa ujumbe umeshatufikia hata kama umeomba radhi hilo ni la mdomoni tu lakini moyoni bado lipo lissu hawezi kuongoza nchi
 
Hongera Ntobi umefanya jumbo jema kujirudi ulitaka kuwapa CCM cha kusema.
 
Ntombi (siyo Ntobi), Yericko Nyenyere (siyo Nyerere), Bonge (siyo Boni) Yai (mwili mkubwa akili kisoda), hawa ni machawa wa Mbowe ambao akili inawaza matumbo yao
ujumbe ulishatufikia lissu hana uwezo alishindwa hata na nyarandu kweliii apewe uenyekiti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…