Ntobi: Heche hawezi kuwa hata mwenyekiti wa mtaa

sonofobia

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2015
Posts
1,171
Reaction score
4,295


Ntobi, mwenyekiti wa Chadema mkoa wa shinyanga na Kijana mtiifu wa Mbowe ameendelea kushambulia wasiomuunga mkono Mbowe.

Safari hii anasema kuwa John Heche hawezi kuwa hata mwenyekiti wa mtaa.

Heche ambaye amewai kuwa mwenyekiti wa bavicha taifa, diwani na mbunge. Kwa sasa vijana wa Mbowe wanatuambia hana sifa za kuwa hata mwenyekiti wa mtaa.
 
Huyu Ntobi huwa anasema/kutenda kabla ya kufikiri. Soon atatoka hadharani na kuomba radhi kama alivyofanya kwa Lisu.

Ni mzee wa kukurupuka.
 
Hiyo ndiyo Chadema ya Mbowe
 
Ntobo ana Matusi sana 🐼
 
migambo wanaruka na kukanyagana sio?

ni muhimu sana muungwana akajibiwa kwa hoja licha ya tafiti kuonyesha heche anafaa zaidi umakamu myekiti Taifa
 
Huyo Ntobi anaidharau Sana. Eti wajumbe wa Mkutano Mkuu tumeahatamba na Wenje. Leo CHADEMA wanamuona mwana CCM Wenje wa maana kuliko Heche.
 
Never trust a politician, uishangae lolote hapo.
Wote ni walewale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…