Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda, ameibua hisia kali mitandaoni baada ya ku-share ujumbe wa kusikitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram. Kupitia posti hiyo, Nuh alieleza machungu anayoyapitia, akifichua hali ngumu inayomkabili, hasa katika mahusiano yake na familia.
Katika ujumbe wake mzito, msanii huyo aliandika:
"Naomba sana kama nikifa asije mama, baba wala ndugu yangu yoyote (yeyote) kunizika mimi. Naomba nizikwe na serikali na mashabiki wangu. Naandika kwa uchungu sana, naamini Mungu anahisi maumivu yangu. Oya, hakuna kitu kibaya kama familia kukuacha na kukuona hauna maana wakati unaamini wao ndio furaha yako ya mwisho..."
Aliendelea kufunguka zaidi kwa kusema kuwa amejitahidi kuacha pombe, lakini kutokana na changamoto kubwa anazopitia, anaona hiyo ndiyo njia pekee inayoweza kumpa furaha kwa sasa.
"Mimi nateseka sio kiuchumi, kuna mengi napitia. Naomba umma ijue na iwe kama njia sahihi na mfano bora kwa vijana wanaopitia changamoto za kifamilia na kimapenzi."