Nuh Mziwanda afunguka machungu ya Maisha adai akifa "asije baba, mama wala ndugu" kunizika! Aomba azikwe na Serikali

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda, ameibua hisia kali mitandaoni baada ya ku-share ujumbe wa kusikitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram. Kupitia posti hiyo, Nuh alieleza machungu anayoyapitia, akifichua hali ngumu inayomkabili, hasa katika mahusiano yake na familia.

Katika ujumbe wake mzito, msanii huyo aliandika:

"Naomba sana kama nikifa asije mama, baba wala ndugu yangu yoyote (yeyote) kunizika mimi. Naomba nizikwe na serikali na mashabiki wangu. Naandika kwa uchungu sana, naamini Mungu anahisi maumivu yangu. Oya, hakuna kitu kibaya kama familia kukuacha na kukuona hauna maana wakati unaamini wao ndio furaha yako ya mwisho..."

Aliendelea kufunguka zaidi kwa kusema kuwa amejitahidi kuacha pombe, lakini kutokana na changamoto kubwa anazopitia, anaona hiyo ndiyo njia pekee inayoweza kumpa furaha kwa sasa.

"Mimi nateseka sio kiuchumi, kuna mengi napitia. Naomba umma ijue na iwe kama njia sahihi na mfano bora kwa vijana wanaopitia changamoto za kifamilia na kimapenzi."

 
Kuzaa watoto ni sawa na upatu mtanielewa siku moja ,Nuh Mziwanda anapata matatizo ila wazazi waliomzaa hawana msaada kwake kabisa ila wanategemea akikaa sawa awatunze hata hao ndugu zake ni hovyo.

Kiuhalisia ifike muda mtu kujiua iwe ni haki na huru kabisa kwa vile dunia haina maana , sometimes unajikuta huendani na mikazo ya dunia ...Kwa kweli wapitishe tu sheria hiyo hakuna ulazima wa kuendelea kushikilia maumivu hata wewe ulizaliwa bila ya ridhaa yako.

Ndio maana yule jamaa wa P square alisema bora kifo kuliko umaskini ,yuko sahihi kabisa kwa nini uendelee kuteseka simply jitoe uhai tu.​
 
Mpe mtengeneza safina huo ujumbe wako.
 
Siyo mama yake tuu, hata baba yake na ndugu zake wote. Huyu anafaa kufukiwa na manispaa kama watakuwa hawajui kwanini ndugu hawamtaki. Vinginevyo atupwe tuu baharini asisumbue marafiki na mashabiki.
Kina baba wengi ni kawaida yao kususa watoto. Ila ukiona mama yako mzazi amekususa inabidi ukae chini ujiulize mara nyingi.
 
Kama anataka apate furaha ya kweli ya moyoni, Hana jinsi zaidi ya kurudi kwenye familia yake.
 
Maana halisi ya depression, Huyu bwana mdogo psychological hayuko sawa kabisa, kuna vitu vingi anaona ameshafeli, afu akiangalia madogo wa 2000 kina Ibra wa konde gang wanatamba mjini
Akubaliane na ukweli kwamba ameshafeli, pombe haitamsaidia zaidi itaendelea kumuangamiza
Afanye ibada Mungu atamfungulia njia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…