Nuhu aliwezaje kuwatambua wanyama wote na kuwaingiza kwenye Safina?

Nuhu aliwezaje kuwatambua wanyama wote na kuwaingiza kwenye Safina?

john achila mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
142
Reaction score
281
Nuhu aliwezaje kuwatambua wanyama wote na kuwaingiza kwenye Safina?

Biblia inatuambia kuhusu kazi aliyopewa Nuhu, ya kuviingiza katika Safina, viumbe virukavyo, vya kiume na vya kike kwa jinsi yake, na kila namna ya wanyama wa kiume na wa kike kwa jinsi yake.
Kitabu cha Mwanzo 7:
2 “Katika Wanyama wote walio safi ujitwalie saba-saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili-wawili, mume na mke,
3 Tena katika ndege wa angani saba-saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote”.

Swali linakuwa, je, Nuhu alipata wapi ujuzi huo wa kuvitambua hivyo viumbe vyote, na je, hao wanyama wote aliwatolea wapi?

Ukisoma kitabu cha Mwanzo 6:20, Biblia inasema: “Katika vyote virukavyo kwa jinsi yake, na kila namna ya mnyama kwa jinsi yake, kila kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake, wawili wa kila namna WATAKUJA KWAKO ILI UWAHIFADHI”.

Unaona hilo neno “WATAKUJA KWAKO ILI UWAHIFADHI”.

Hiyo ni kuthibitisha kuwa siyo wanyama wote Nuhu alikwenda kuwachunguza kujua jinsia zao au kuwakamata, hapana. Wengine walikuja wenyewe. MUNGU MWENYEWE NDIYE ALIYEWAPELEKA kwenye Safina, isipokuwa wale wa kufugwa, ambao wao wanajulikana.

Wengi wa hao waliosalia, Mungu aliwapeleka mwenyewe kwa Nuhu
.

Kazi ya Nuhu ilikuwa ni kuwaingiza tu ndani ya Safina, ambayo ilikuwa ni ya gorofa tatu.

Hiyo inaonyesha ukuu na uweza wa Mungu.

Kinachoshindina kwa binadamu, kwa Mungu hakuna kinachoshindikana.
 
Tangu Mwanzo Mungu amempa mwanadamu akili ya kutambua wanyama na kuwaita Majina,
(Mwanzo2:19-20)
Nasi kama uzao wa Adamu tuna akili hiyo hiyo ya kutambua viumbe na kuviita majina.
 
Hiyo story ni fiction, hakujawahi kuwa na gharika ya dunia nzima.
 
Muamini Mungu lakini usiamini kila kilicho andikwa kwenye biblia.
 
Biblia ilianza uongo mapema sana katika kitabu cha mwanzo kabisa,huku Qu.ran yenyewe ikiwa ndio haina maana kabisa ikikopi kila neno la kwenye biblia na kubadilisha tu kidogo maneno
 
Ile ilikuwa ni EL NINO ya kipindi hicho iliyolikumba eneo la Mashariki ya Kati
 
Back
Top Bottom