Nukuu ya Dkt. Bashiru: "Madalali wa mali za Umma hawawezi kupendezwa na kuhojiwa"

Source tafadhali. Usije ukamlisha maneno Mzee wa watu
 
Niamini, hata huo Ubunge aliompa hawezi hata kumnyang'anya!

Zingatia; Kuwa CS hata ndani ya wiki moja tayari hiyo ni habari nyingine.
Hatemeshwi na mtu ubunge, sasa akiwa hana income, madeni atalipa vipi?


Hivi wewe unaijuwa pangani au unaisikia tu?

Ulishaona wapi Tanzania hii Katibu Mkuu wa CCM akaenda kuwa mbunge? Aisee, yale ni matusi.

Katibu Mkuu wa CCM Tanzania ana power kuliko Makamo wa Rais au Waziri Mkuu, anaweza kuwaita hao ofisini kwake na wakavunja kazi zao zote wakenda mbio kumsikiliza.
Sijui uko upande gani kipindi cha magu ulikuwa ukisema wasafi hawa leo .mama tena msafi kifupi ww uko na serikali hata ikiamua iwe ya mashoga
Mwendazake nilimsifia sana mwanzoni. Duh, alipovuwa ngozi ya kondoo na kuonesha vazi lake halisi nikamuona hafai kabisa.

Alipotea stepu sana kulewa Madaraka mapema.
 
Huyu ni ndg yetu lakini ktk imani, umesahau?!.
 
Hii italeta makasiriko
 
Bila shaka ww ni mke wa mhuni mmoja hivi ndo maana kipindi hiki umekuwa na sauti
 
Maskini kaprofesa kamekua kadogo kama sisimizi. Ama kweli ukiniliwa Kuwa Myenyekevu. Ukijikweza utashushwa na kufedheheka sana...
 
Almanusura nikutag huu uzi. Kumbe ushafika fasta

Nadhani kwa level yako kuanza kumuassassin CS mstaafu ni kujikwaa.

Hebu tujadili alichokisema kama kina usahihi namna gani na hakina usahihi kivipi. Leo tunazungumzia DP World kama tunavyoshabikia Simba na Yanga. Nimejiuliza kwa nini Serikali ime mute kuuelimisha umma kwa uwazi kuhusu hitaji na faida za kuingia huo Mkataba unaoitwa Makubaliano?

Kwa nini wanaoukosoa wanapewa tuhuma kuwa wanatetea matumbo yao na si maslahi ya umma?

Napenda Maendeleo lakini si ya hila. Tuangalie mustakabali wa Taifa tena kwa tahadhari zote. Tusilazimishe jambo ambalo manung'uniko ni mengi.

Tumsaidie Rais kutimiza wajibu wake na si kumuwekea mitego ya kisiasa
 
Hayo maneno yalisemwa tarehe 12 October 2018 Mh Bashiru. Msituchanganye... Bashiru kajikalia kimya Mzee wa watu.
 
 
Wazee wa atake asitake tutamuongezea muda kwenye ubora wao,teh teh teh
 
Samia ni dalali?
Samia chaguo la Mwenyezi Mungu.

Yule mama katuokowa sana Tanzania kiuchumi. Mungu ampe umri mrefu wajomba zake walimsikiliza 2020 wakamuenzi.

AlhamduliLlah Mzee Mwinyalienda. Kumpa ushauri mwendazake akamuelewa, akamtuma mama nchi za Kiarabu.

Na alipokwenda huki wajomba sijuwi Ammi zake hawakumuangusha.

Arab Contractors waliliopwa hukohuko juu kwa juu dakika hiyo hiyo, Waturuki nao ndiyo hayo hayo.


AlhamduliLlah wskaanza tena kazi, miradi ilishasimama hiyo.


Waulize waliopo front wakwambie nini kilitokea 2019/20. Kwenye hiyo miradi.


Oesa zote zinazokopwa zilienda kwenye kampeni, ikawa jamaa hawalipwi wanazungushwa, wakaanza kujiondoa mdogo mdogo.


Jamani serikali zina mengi sana nyuma ya pazia, msione watu wanajimwambafai halafu wanapewa kavu za uso mkaona ni kawaida tu. Ujuwe hapo mtu kishapigwa roba la nguvu, hana ujanja.
 

Mwendazake aliwapoteza wengi sana
 
Tunafahamu inawachoma sana.

Na bado.

Wana chuki zisizo na kifani,it's too bad itawauwa Kwa presha na visokolokwinyo vyao, because madam president tunae had 2030 Inshallah katika kuiletea mama Tanzania maendeleo.
 
Mnafiki tu huyu, mbona ripoti ya Wezi wa Mali za CCM hakuweka hadharani.
 

F.F,
Hawawez elewa mambo kama hayo,hao wanadhan kuongoza nchi ni kama ni jambo rahis tuh kama kuongoza kile chumba Cha mtaa wa ufipa pale,nchi Ina mambo mengi na makubwa,

Samia amepokea kijit katika mazingira magum na amefanya reforms nyingi kutengeza balance ndan ya nchi ili mambo yaende,kimoyo moyo wanakubali hawa sema tuh chuki na nongwa zao za asili ndizo zinazowasumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…