Nukuu za Rais Samia katika kilele cha wiki ya UWT

Nukuu za Rais Samia katika kilele cha wiki ya UWT

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
NUKUU ZA RAIS SAMIA KATIKA KILELE CHA WIKI YA UWT.

"Tumekutana hapa kwa madhumuni makuu mawili, moja ni kuadhimisha kilele cha Wiki ya UWT Kitaifa na jambo la pili ni kumuenzi Hayati Bibi Titi Mohamed na tena aenziwe hapa nyumbani kwake Rufiji"

"Historia ya Bibi Titi Mohamed imeandikwa katika kurasa chache sidhani kama imetosha. Nitoe rai kwa watafiti na waandishi wa masuala ya siasa na jamii wafanye hivyo ili jamii iweze kuujua mchango wa marehemu Bibi Titi Mohamed kwa jamii na Taifa"

"Tumekusanyika hapa si tu kumsifu ili tumsifu, bali tumsifu kwa lengo la kwenda kujipaga kwa matendo yetu yaendane na dhamira ya shujaa wetu huyu Marehemu Bibi Titi" Rais Samia Suluhu Hassan

"Wito wangu kwa wanawake, kuendelea kuwa wamoja na kurekebishana mapungufu tuliyonayo kwa njia ya vikao na njia za kistaarabu,"

"Biblia imetupa ruhusa wanawake tuseme, lakini kwenye Biblia tuliambiwa tuseme mema, sasa wanawake sisi hatuitumii vyema hiyo fursa, Biblia imetutuma tubebe mema tuyatangaze kwa watu, sisi tunakwenda kutangaziana uovu, kuzushiana majungu na kusambaza umbea,"

"Sasa naomba mjue kwamba hiyo ni dhambi, turudi kwenye maagizo ya Biblia lakini nina hakika dini zote zimetuelekeza hivyo kusema yaliyo mazuri na tusiseme yale ya uongo, majungu, uzushi na kusambaziana yasiyokuwepo"

#WikiYaUWT
#KilelechaWikiyaUWT
#BibiTitiAenziwa


IMG-20211023-WA0052.jpg
 

Mtemi Hangaya,

Katika Biblia hiyo hiyo; amri ya tisa inasema "Wala usimshuhudie jirani yako uongo". Kum 5:20

 
Back
Top Bottom