Masoko mengine kwa china ni kama ALIEXPRESS, ALIBABA n.k
JE NITAUPATA VIPI MZIGO WANGU BAADA YA KUWA UMEFIKA TANZANIA?
- Utapigiwa simu kukujulishwa kuwa mzigo wako umefika.
- Utaletewa ofisi kwa wale wanaoishi katikati ya jiji ya Dar es salaam, FREE DELIVERY. au
- Utaelekezwa mahala unatakiwa ufike ili uchukua mzigo - Ni city centre kwa walio Dar es salaam, Waweza kuja wewe mwenye au ukamtuma mtu akuchukulie.
- Kwa walio mikoani au nje ya Tanzania utatumiwa kwa njia ya EMS au kwa njia ya basi kwa kadri wewe utakavyo pendekeza njia ipi itumike – Utalipia hii ghalama.
Mifano hai:
1. Mteja Toka nje ya TZ (anaishi DRC) – Bidhaa yake imetoka China, Na alitumia kwa basi kwenda DRC.
2. Mteja ndani ya TZ anaishi Mkoani – Bidhaa yake imetoka UK
Wateja wote nimekutana nao hapa JF na hakuna tuliye onana ana kwa ana, Zaidi ya njia za mawasiliano tajwa hapo juu.
ANGALIZO
1. Usifanye malipo yeyote bila kuwasiliana nami kwanza, Kwa njia mojawapo ya mawasiliano tajwa hapo juu.
2. Haito tokea kupigiwa simu, au kuandikiwa ujumbe mfupi, kuwa fanya malipo kwenda namba Fulani ya simu.
3. Hakuna malipo yeyote yatakayofanyika kwa fedha taslimu kwa kukabidhiana mkononi.
4. Malipo yote ya fedha yatafanyika kwa utaratibu uliowekwa hapo juu.
5. Miongoni mwetu kuna wenye uoga na mawazo ya kuibiwa/ kutapeliwa pindi lijapo swala la fedha na swala zima la manunuzi mtandaoni.
Yaani kutuma fedha kwa mtu usie mfahumu/ kumuona/ asiye na ofisi mahala ulipo.
Na hujibainisha kwa haya maswali Ofisi yako iko wapi? , Uko wapi nataka nikukabidhi fedha mkononi au nataka tuandikishiane!
- ONDOA shaka, kwa kufuata taratibu zilizo ainishwa hapo juu, uko salama, Na bidhaa yako AU huduma utakayolipia utaipata.
- Iwapo UNA SWALI, PENDEKEZO au USHAURI wasiliana namI au andika kwenye hii thread.
Ndege - Huchukua wiki 3, kufika, ila ghalama ya usafirishaji ni kubwa angalia post namba moja.
Meli - Huchukua muda mrefu kufika wiki 6 - Ila ghalama ya usafirishaji ni ndogo sana, hasa kama unachukua mzigo mkubwa mfano vifaa vya ujenzi, Usafiri wa meli ni sahihi.
Baada ya kuwa tumekubaliana 1. Idadi ya taa, 2. Njia ya usafirishaji, Nitakupa gharama kamili ya kiasi unachotakiwa kulipia na utachagua njia ya malipo mojawapo (angalia post ya kwanza).
MUDA WA KUWASILIANA NAMI
1. 06:00 – 19:30hr (Saa 12:00 asubuhi HADI Saa 1:30 Usiku)– Simu/sms/whatsapp/telegram - Utajibiwa
2. 19:30 – 06:00hr (Saa 1:30 usiku HADI Saa 12:00 asubuhi)– Niachie ujumbe wa simu (sms)/whatsapp/telegram/email, Na utajibiwa au kupigiwa simu kabla ya 08:00hr Kila siku.
1. Fungua google.com
2. Andika kiusahihi item unayohitaji malizia na neno "from Japan"
3. Kagua lnk tatu za kwanza
4. Nipe link ya bidhaa utakayokuwa umechagua
5. Mchakato wa kujua ghalama utafanyika
Angalizo: Unachokifanya sio njia sahihi ya kutangaza hiyo webste yako hapa JF. Tafuta njia nyingine. Japo sasa unatumia ID ya march 2, (Mar 2, 2024) ila tambua ninakufahamu vizuri sana. Makinika.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.