Kifaranga
Senior Member
- Jan 6, 2011
- 144
- 31
Mchanganuo mwingine ktk kuwekeza kwenye mashine za kutotolesha vifaranga. Je itarudisha gharama zako?
Hebu soma kwa makini mchanganuo huu:
Hebu tuchukulie umewekeza takribani, (2,000,000sh) kwenye mashine ya mayai 528. Utakuwa na uwezo wa kuzalisha takribani 176 vifaranga kwa wiki. Gharama zako hasa zitakuwa kwenye mayai yaliyorutubishwa na umeme. Hapo tuchukulie umekupata mayai yaliyorutubishwa kwa (400sh)@ mayai na (50sh) kama umeme utakaotumia kwa YAI, hivyo jumla ya gharama za kuzalisha kifaranga ni wastani (450sh Kifaranga. Kama utauza vifaranga vyako vyenye siku 1 kwa (1000sh) (makadirio ya haraka, inaweza kuwa zaidi), utatengeneza faida ya (550sh) @ kifaranga. Kama ukizidisha (550sh) kwa mayai 176 kwa wiki, utakuwa umetengeneza (96,800sh) kwa wiki. Sasa chukua mtaji wako uliowekeza awali wa (2,000,000sh) ugawanye kwa faida yako ya kila wiki ya (96,800sh), utarejesha gharama zako ulizowekeza awali ndani ya kipindi cha wiki 20 = miezi 5. Kama utabadilisha kidogo hizo namba hapo juu, utakuta muda mrefu kabisa utakaochukua kurejesha gharama zako za awali ulizowekeza itakuwa miezi 6. Hivyo jibu ni kati ya miezi 4 mpaka miezi 6 imechelewa sana mwaka 1 baada ya hapo ni faida tutu.
Unaweza kutengeneza kipato zaidi ya hapo kwa kufanya biashara ya kutotolesha mayai, na kuzalisha vifaranga kasha kuwalea na kuwauza kama kuku wazima. Kiukweli gharama zako zitarudi mapema zaidi na Kupata faida na faida. Be smart and make smart investment.
Aiseeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee