Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 25,186
- 27,366
Mahakama ya Mkoa wa Lindi imemhukumu Nurdin Mwanga, mkazi wa Mnolela, kwenda jela miaka 30 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumbaka Mwanafunzi wa Sekondari mwenye umri wa miaka 16.
Hukumu hiyo imetolewa Oktoba 08, 2026, katika Kesi Na. 19961 ya mwaka 2026, na Hakimu Mkazi Deliphine Kimati, baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka.
Upande wa mashtaka, uliowakilishwa na Mawakili wa Serikali Godfrey Mramba na Mofati Seth, uliwasilisha Mahakamani mashahidi sita pamoja na vielelezo vitatu.
Ilielezwa Mahakani hapo kuwa mwanafunzi huyo alitoweka nyumbani kwa wazazi wake Aprili 26, 2026, na baada ya juhudi za kumtafuta, alibainika Mei 05, 2026 akiwa na mtuhumiwa huyo, ambapo walikuwa wakiishi pamoja katika nyumba moja.