Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
NUREMBERG TRIALS
Hii ilikuwa mahakama iliyokuwa Ujerumani baada ya Vita Kuu ya Pili (1939 - 1945) washirika wa vita vile dhidi ya Manazi wa Kijerumani waliiweka makhsusi kwa kuwahukumu wale wote walioua watu katika vita vile.
Kwa hakika Washirika hawa wakiongozwa na Marekani na Waingereza ile mahakama iliwekwa tu iwepo lakini walikuwa weshaamua kuwaua wale wote waliokuwa viongozi katika katika utawala wa Hitler ingawa wenyewe ukiwaambia hili watakataa watadai kuwa wao wanafuata sheria hawawezi kuua watu bila kuwafikisha mahakamani.
Dunia ilikamatwa na uchungu mkubwa kwa yale ambayo yalifanyika katika kambi za mauaji na mateso walizoweka Wajerumani maarufu ikiwa ni kambi iliyokuwa Auschwitz, Poland.
Katika kambi hii kulikuwa na vyumba vya kuwaua Wayahudi kwa kutumia gesi ya sumu.
Hii Wajeruami waliona ni njia bora tena ya ''safi,'' ambayo hachafuki mtu.
Taarifa zilipenya wakati vita inaendelea na zikawafikia Waingereza na Wamarekani na Washirika wengine kuwa Manazi wanaua watu kwa halaiki lakini ilikuwa tabu kuamini kuwa kuna binadamu anaeweza kufanya kitu kama hicho.
Katika kambi hizi ilikuwa kazi ngumu na chakula kidogo na haupiti muda mfungwa anakufa kama mbwa.
Wajerumani walipojua kuwa sasa wanashindwa vita Red Army iko mpakani jeshi linaelekea Berlin wakawa sasa wanajitahidi kufuta ushahidi wa ule unyama walioufanya.
Lakini wapi hawakuweza.
Majeshi ya Washirika walipofika Auschwitz macho yao hayakuweza kuamini kile walichokuwa wanakiona mbele yao.
Binadamu anatembea ni ngozi na mfupa hana misuli.
Mbavu zimebana tumbo unahesabu pingili za uti wa mgongo.
Waliyoyaona ndani ya vile vyumba vya gesi hakuna aliyeweza kuyaeleza.
Hapa ndipo Washirika walipoamua lazima wawaue Manazi wote na wale waliowasaidia iwepo mahakama isiwepo mahakama hakuna atakaebakishwa.
Akili ya binadamu iliyosalimika ikawa inajiuliza binadamu anaweza vipi kumfanyia binadamu mwenzake unyama kama ule?
Picha za ushenzi ule zilipoenea dunia nzima kila mtu alilizwa na yale yaliyowakuta Wayahudi katika mikono ya Manazi.
Manazi waliopelekwa mahakamani walijitetea kuwa wao ni askari wakitii amri lakini wakatambua mapema sana kuwa utetezi huu hauna maana yoyote pale mahakamani.
Wakahama katika utetezi huu ikawa sasa wanajifanya kuwa wamepoteza kumbukumbu hawawezi kukumbuka yale yaliyotokea mwaka wa 1939 au 1942 nk.
Haikusaidia kitu.
Wakauliwa kwa amri ya mahakama na haikutokea hata nchi iliyowaombea msahamaha.
Viongozi wetu bado wana muda wa kujifunza katika historia hii achilia mbali katika yale yaliyofanyika wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar na baada ya Mapinduzi na yale mauaji yaliyotokea 2001 baada ya uchaguzi.
Tuna uzoefu wa kutosha kuturekebisha na kujua kuwa Zanzibar haiwezi tena kubeba historia nyingine ya kumwagika kwa damu ya wananchi wake.
Lakini sisi hii leo tanaposikia maneno ya kutisha ya kuua na mfano wa hayo yakitolewa na vijana ndani ya vyama vya siasa tukielekea katika uchaguzi hivi hatujiulizi tumefikafikaje katika hali hii?.