Nuremberg trials

Nuremberg trials

Sasa wewe kwa akili yako unaamini kulikuwa na mauaji ya kimbari dhidi ya Mayahudi au ni propaganda tu? Hivi kwa population ya Mayahudi kipindi hicho wangeuawa milioni tano kungekuwa na Myahudi aliyesalia duniani hivi sasa? Kama kuna ukweli mbona hakuna tume yoyote huru iliyoundwa kuchunguza jinai hiyo na kila anayetaka kuchunguza au kuzungumza kinyume anawekewa vikwazo? Kuna Gypsies na Roma pia waliuawa kwa maelfu wakati wa WW2 mbona wao hakuna anayewazungumzia zaidi ya Mayahudi? Sipingi kuwa Mayahudi waliuawa kwenye WW2 lakini si kwa kiwango kinachosemwa ni propaganda tu hizo ili kulinda maslahi ya Mayahudi.
Pili, nikukumbushe tu kuwa Nuremberg trials hazikuwa tu kwa mauaji ya kimbari bali mashtaka mengine kama crimes against peace, crimes against humanity and war crimes yalisikilizwa ambapo pia Allies committed such atrocities. Mahakama ya Nuremberg ilikuwa ni victors justice against the vanquished.
Mkuu, hebu tuwekane sawa kidogo hapa. Mauaji ya kimbari (Crime of Genocide) huwa hayaangalii idadi ya watu ambao wameuawa bali nia ya mauaji hayo (The Intention of the perpetrator). Ndiyo maana unaweza usitekeleze uuaji, lakini bado ukafungwa kwa kosa la kupanga mauaji ya kimbari (Conspiracy to commit genocide).

Pili, kosa la mauaji ya kimbari kule Nuremberg lilikuwepo. Tofauti ni kwamba mpaka kufika mwaka 1948 mauaji ya kimbari (Crime of Genocide) yalikuwa ni sehemu ya kosa la Mauaji dhidi ya ubinadamu (Crimes against humanity).

Lakini baada ya wakina Raphael Lemkin kuandika kuhusu Genocide, na mwaka UNO 1948 tukatengeneza The Genocide Convention, ndiyo kosa la Genocide likaanza kujitegemea.


Mbali na hapo, hoja yako ni nzuri sana na inafanya mtu ajifikirie zaidi juu ya mambo mengi tunayoaminishwa kwenye historia.
 
Ukianzisha vita na ukashindwa lazima ulipe gharama.Adolf Hitler kosa lake ni kianzisha vita na kukiuka sheria za kimataifa.Stalin na Mao waliua watu wengi lakini wao hawakuanzisha vita.
Mkuu uvamizi dhidi ya Poland mnamo Septemba 1939 ulifanywa kwa pamoja na Ujerumani na USSR. Ina maana Stalin pia alikuwa aggressor na lipaswa kuwajibishwa. Narudia tena, Nuremberg trials were a victors' justice against the vanquished.
 
Shida ilianza walipomuacha Solemba Farao kule Egypt. Sababu walipendelewa kujua elimu fulani adimu, waliishi kama ni watu special. Wanafanya kazi sana. Wabunifu sana. Wanafuata culture na dini yao sana. Sisi watu wa mataifa hatupendi hizi akili nyingi
Akili nyingi watoe wapi!!!...huwezi kuwa na akili nyingi kisa ni dini au kabila
 
Akili nyingi watoe wapi!!!...huwezi kuwa na akili nyingi kisa ni dini au kabila
Hatuongei kama wanywa kahawa wa Gerezani. Myahudi ana statistics zinambeba. Ndio maana anachukiwa. Sisi wengine tunywe kahawa...halafu tunywe uji wa ulezi...halafu tunywe alkasusu...tukajambe na kulala
 
Hatuongei kama wanywa kahawa wa Gerezani. Myahudi ana statistics zinambeba. Ndio maana anachukiwa. Sisi wengine tunywe kahawa...halafu tunywe uji wa ulezi...halafu tunywe alkasusu...tukajambe na kulala
Kuna waethiopia ni wayahudi pia...hebu lete ushahidi kwamba Wana akili Sana,ukiambatanisha na tafsiri ya akili
 
Kuna waethiopia ni wayahudi pia...hebu lete ushahidi kwamba Wana akili Sana,ukiambatanisha na tafsiri ya akili
By large and far... Have you heard about the story of Ethiopian Jews who were taken back to Israel in 80s? Namba haziongopi. Sioku tukibadili kufikiri mambo yatakuwa mazuri sana
 
By large and far... Have you heard about the story of Ethiopian Jews who were taken back to Israel in 80s? Namba haziongopi. Sioku tukibadili kufikiri mambo yatakuwa mazuri sana
Unadhihirisha utumwa wako kwa kutumia lugha ngeni,mtumwa wa kifikra
 
Mkuu unatulisha matango mwitu. Japan ilisalimu amri kushindwa vita hiyo negotiation ya amani ilitoka wapi?
Jidanganye,unafikiri kwanini Hirohito alibaki kuwa mfalme wa Japan hadi 1989 alipofariki? Kila vita inapoisha huwa Kuna makubaliano .Vita haiishi bila makubaliano,1979 Idd Amin alipokimbia Uganda unajua kwanini majeshi ya Tz yalibaki huko zaidi ya miaka miwili?
 
NUREMBERG TRIALS

Hii ilikuwa mahakama iliyokuwa Ujerumani baada ya Vita Kuu ya Pili (1939 - 1945) washirika wa vita vile dhidi ya Manazi wa Kijerumani waliiweka makhsusi kwa kuwahukumu wale wote walioua watu katika vita vile.

Kwa hakika Washirika hawa wakiongozwa na Marekani na Waingereza ile mahakama iliwekwa tu iwepo lakini walikuwa weshaamua kuwaua wale wote waliokuwa viongozi katika katika utawala wa Hitler ingawa wenyewe ukiwaambia hili watakataa watadai kuwa wao wanafuata sheria hawawezi kuua watu bila kuwafikisha mahakamani.

Dunia ilikamatwa na uchungu mkubwa kwa yale ambayo yalifanyika katika kambi za mauaji na mateso walizoweka Wajerumani maarufu ikiwa ni kambi iliyokuwa Auschwitz, Poland.

Katika kambi hii kulikuwa na vyumba vya kuwaua Wayahudi kwa kutumia gesi ya sumu.

Hii Wajeruami waliona ni njia bora tena ya ''safi,'' ambayo hachafuki mtu.

Taarifa zilipenya wakati vita inaendelea na zikawafikia Waingereza na Wamarekani na Washirika wengine kuwa Manazi wanaua watu kwa halaiki lakini ilikuwa tabu kuamini kuwa kuna binadamu anaeweza kufanya kitu kama hicho.

Katika kambi hizi ilikuwa kazi ngumu na chakula kidogo na haupiti muda mfungwa anakufa kama mbwa.

Wajerumani walipojua kuwa sasa wanashindwa vita Red Army iko mpakani jeshi linaelekea Berlin wakawa sasa wanajitahidi kufuta ushahidi wa ule unyama walioufanya.

Lakini wapi hawakuweza.

Majeshi ya Washirika walipofika Auschwitz macho yao hayakuweza kuamini kile walichokuwa wanakiona mbele yao.

Binadamu anatembea ni ngozi na mfupa hana misuli.

Mbavu zimebana tumbo unahesabu pingili za uti wa mgongo.

Waliyoyaona ndani ya vile vyumba vya gesi hakuna aliyeweza kuyaeleza.

Hapa ndipo Washirika walipoamua lazima wawaue Manazi wote na wale waliowasaidia iwepo mahakama isiwepo mahakama hakuna atakaebakishwa.

Akili ya binadamu iliyosalimika ikawa inajiuliza binadamu anaweza vipi kumfanyia binadamu mwenzake unyama kama ule?

Picha za ushenzi ule zilipoenea dunia nzima kila mtu alilizwa na yale yaliyowakuta Wayahudi katika mikono ya Manazi.

Manazi waliopelekwa mahakamani walijitetea kuwa wao ni askari wakitii amri lakini wakatambua mapema sana kuwa utetezi huu hauna maana yoyote pale mahakamani.

Wakahama katika utetezi huu ikawa sasa wanajifanya kuwa wamepoteza kumbukumbu hawawezi kukumbuka yale yaliyotokea mwaka wa 1939 au 1942 nk.

Haikusaidia kitu.

Wakauliwa kwa amri ya mahakama na haikutokea hata nchi iliyowaombea msahamaha.

Viongozi wetu bado wana muda wa kujifunza katika historia hii achilia mbali katika yale yaliyofanyika wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar na baada ya Mapinduzi na yale mauaji yaliyotokea 2001 baada ya uchaguzi.

Tuna uzoefu wa kutosha kuturekebisha na kujua kuwa Zanzibar haiwezi tena kubeba historia nyingine ya kumwagika kwa damu ya wananchi wake.

Lakini sisi hii leo tanaposikia maneno ya kutisha ya kuua na mfano wa hayo yakitolewa na vijana ndani ya vyama vya siasa tukielekea katika uchaguzi hivi hatujiulizi tumefikafikaje katika hali hii?.
Israel anachofanya Palestine atafikishwa kwenye hizo mahakama kweli.Sheria ni msumeno.
 
Back
Top Bottom